Wakulima wakiwa katika shughuli za kilimo cha pamba:
NA AHMAD NANDONDE RORYA.
Walimu pamoja na wanafunzi wa shule
ya msingi Nyamasieki wilayani Rorya mkoani Mara wameanzisha shamba darasa la zao
la Pamba kama sehemu ya kufanya majaribio ya kilimo cha zao hilo litakalokuwa
likilimwa kwa njia ya kisasa na hivyo kuwasaidia wakulima wilayani humo kutafuta
zao la biashara na hivyo kusaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi
kupitia zao hilo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyamasieki
Bw. PETER EXAVERY amesema baada kufanikiwa katika jaribio la kwanza la ulimaji
wa zao hilo msimu uliopita uongozi na wanafunzi wa shule hiyo wameamua kuongeza
hekari 21 ili kukiendeleza kilimo hicho.
Aidha ameongeza kuwa mapato
yatokanayo na zao hilo yatasaidia kutatua mahitaji ya chakula kwa wanafunzi shuleni
hapo.
Kufuatia ubunifu uliofanywa na
viongozi na wanafunzi wa shule hiyo mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM wilayani
humo DAVID IRANGA amewaomba wananchi kuacha kulalamikia ugumu wa maisha na
badala yake waige mfano ulioneshwa na shule hiyo ili kujikwamua kiuchumi.
Mwishoo...
KILIMO NI AJIRA EWE MWANANCHI KIMBILIA FURSA HIII SASA:
0 comments:
Post a Comment