`

WANAFUNZI WAUNGANA NA WALIMU WAO KUANZISHA SHAMBA LA MFANO LA PAMBA


 
     wakulima katika shughuli zao za kilimo:                            
Wakulima wakiwa katika shughuli za kilimo cha pamba:


           Pamba iliyokomaa kabla ya kuvunwa:

          Pamba iliyovyunwa tayari kwa kupelekwa sokoni:
NA AHMAD NANDONDE RORYA.

Walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Nyamasieki wilayani Rorya mkoani Mara wameanzisha shamba darasa la zao la Pamba kama sehemu ya kufanya majaribio ya kilimo cha zao hilo litakalokuwa likilimwa kwa njia ya kisasa na hivyo kuwasaidia wakulima wilayani humo kutafuta zao la biashara na hivyo kusaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi kupitia zao hilo.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyamasieki Bw. PETER EXAVERY amesema baada kufanikiwa katika jaribio la kwanza la ulimaji wa zao hilo msimu uliopita uongozi na wanafunzi wa shule hiyo wameamua kuongeza hekari 21 ili kukiendeleza kilimo hicho.

Aidha ameongeza kuwa mapato yatokanayo na zao hilo yatasaidia kutatua mahitaji ya chakula kwa wanafunzi shuleni hapo.

Kufuatia ubunifu uliofanywa na viongozi na wanafunzi wa shule hiyo mwenyekiti wa umoja wa vijana CCM wilayani humo DAVID IRANGA amewaomba wananchi kuacha kulalamikia ugumu wa maisha na badala yake waige mfano ulioneshwa na shule hiyo ili kujikwamua kiuchumi.
Mwishoo...
 KILIMO NI AJIRA EWE MWANANCHI KIMBILIA FURSA HIII SASA:




FUATILIA MKASA WA KUSISIMUA WA KIJANA FABBY KUTOKA MKOANI MTWARA SEHEMU YA KWANZA


FABI KIJANA KUTOKA MKOANI MTWARA…


FABI SIKU MOJA AKIWA ANACHIMBA JALALA AKIWA NA WENZAKE WAWILI NA WAKATI HUO ILIKUWA NI ZAMU YAKE KUWA SHIMONI WAKATI ANACHIMBA GHAFLA NDANI YA SHIMO LA JALALA ALILIGONGA JIWE GHAFLA JIWE LILE LILIANZA KUTOA DAMU NA KISHA UKATOKA MWANGA MKALI SANA HAPO HAPO FABBY AKAANGUKA NDANI NA KUZIMIA WENZAKE WAKIWA NJE YA SHIMO NA STORI ZIMENOGA BAADA WANASHANGAA UKIMYA SHIMONI NDIMO KUMCHUKUA NA KUMPELEKA NDANI.
 
FABI AKIWA AMELALA KITANDANI GHAFLA ANASHTUSHWA NA WANGA MKALI AMBAPO WAKATI HUO AKIWA AMEZUNGUKWA NA WATU WENGI PALE KITANDANI IKIWA NI PAMOJA NA MAMA YAKE WANAULIZANA KULIKONI BASI KATIKA ULE MWANGA ANASEMA ALIKIONA KIUMBE KINACHOFANAN NA MSICHANA MREEMBO AKIWA AMEVAA MAVAZI MITHILI YA MASISTA WA KIDINI NA YULE KIUMBE ALISOGEA MPAKA PALE KITANDANI NA AKANYOOSHA MKONO AKAMSHIKA KTK PAJI LA USO AKAWA KAMA MTU ANAYEMUOMBEA.
 

LAKINI FABI ANASEMA ALIONEKANA KAMA ANASALI LAKINI ILE LUGHA HAKUIFAHAMU LICHA YA KUHISI KAMA ANAOMBEWA..GHAFLA YULE KIUMBE ALITOWEKA. FABBY AKASHTUKA KUTOKA USINGIZINI NA ALIPOKUA AMEKAA KITANDANI AKAJIKUTA AMEZUNGKWA NA UMATI WA NDUGU LAKINI ALIPOWAULIZA KUHUSIANA NA YULE KIUMBE ALIYEKUWA MLE NDANI KILA MTU AKAWA ANAMSHANGAA YEYE BASI FABI AKAGUNDUA ALICHOKIONA ALIKUWA ANAKIONA PEKE YAKE.
 

BASI KUANZIA HAPO YAKAWA YANATOKEA MATUKIO YA AJABU AJABU HADI ALIPOTOKA KWAO AKAWA AMEPANGA MTAA MWINGINE KAMA UNAVYOJUA KIJANA UMRI UKIWADIA..LAKINI SIKU MOJA AKIWA ANATOKA KAZINI ALIPOFIKA NA KUFUNGUA MLANGO WANGE ULIOKUWA UMEFUNGWA NA KUGULI GHAFLA NDANI ANAMKUTA BINTI MMOJA AMELALA KITANDANI KWAKE..BINTI HUYO ALIYEKUWA NA UZURI WA PEKEE NA ALIYEPELEKEA HATA HALI YA CHUMBA KUKIONA TOFAUTI, BASI JAMAA AKIWA AMESIMAMA MLANGONI BINTI HUYO AKAWA ANAAMKA PALE KITANDANI AKIWA KAMA MTU ALIYEBANWA VICHEKO.
 

FABBY ALIPOMTAZAMA JAMAA ALIGUNDUA KIUMBE HUYU NI TOFAUTI NA YULE ANAYEMTOKEA AKIWA NA MAVAZI YA KISISTA (KISISTA WA KANISANI) NA KIUMBE HUYU NDO MTATA ZAIDI AMBAPO ALIANZA KUKUTANA NA MENGI.
 
JE! NINI KITAFUATA? USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA…...UHONDO NDYI KWANZA UNAANZA

VIDEO MVUA KUBWA ILIVYOHARIBU MIUNDOMBINU YA SHULE MBILI NA MAKAZI YA WATU MJINI MUSOMA...



MVUA kubwa iliyoambatana na upepo mkali imenyesha usiku wa kuamkia leo na kuharibu vibaya miundombinu ya umeme, makazi ya watu yakiwemo madarasa 7, ofisi za walimu, maabara na hostel katika shule ya msingi na sekondari ya Kiara zilizopo manispaa ya Musoma mkoani Mara hali iliyozua taharuki kwa wakazi maeneo hayo wakiwemo walimu na wanafunzi wa shule hizo. 
 

Yanga yafanya kikao kizito kuiua St. Louis




By:CHAGABOY
Saa chache kabla ya pambano lao dhidi ya St. Louis, benchi la ufundi na wachezaji wa Yanga wamekaa kikao cha takribani saa moja na nusu kuweka mikakati ya mwisho ya kuwamaliza wapinzani wao.
Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Reef Holiday ambako timu hiyo imefikia tangu ilipofika Shelisheli.
Kikao hicho cha kupeana mikakati na mbinu za kiufundi, kiliongozwa na Kocha Mkuu, George Lwandamina na wasaidizi wake Nsajigwa Shadrack na Noel Mwandila.
Hali ya usiri ilitawala katika kikao hicho kwani zaidi ya wahusika, hakuna mtu mwingine aliyeruhusiwa kuhudhuria.


VIDEO: Okwi awapeleka Simba Misri



By: CHAGABOY

Mchezaji wa simba raia wa Uganda Emmanuel Okwi ndiye ailiyeibuka kinara leo katka mechi ya marudiano kati ya Gendarmarie na Simba iliyopigwa hii leo,Huku mshambuliaji huyo akiipatia Simba goli kunako dadika ya 55 kipindi cha pili na kuifanya Simba kuibuka na usindi wa bao moja .Na hivyo kuifanya Simba kusonga mbele katika michuan ya kombe la shirikisho Africa


Audio | Nikki Mbishi – Nimekumiss | Mp3 Download

Audio | Nikki Mbishi – Nimekumiss



Audio | Lava Lava – Utatulia (Piano Version) | Download Mp3

Audio | Lava Lava – Utatulia (Piano Version)


YALIYOJIRI SHINYANGA KATIKA MECHI YA SIMBA NA MWADUI LEO KATIKA VPL



MPIRA UMEKWISHAAAAAAA

-KADI Sangija analambwa kadi ya njano kwa kuzuia mpira haujapigwa
-Krosi ya Kichuya, mpira unaokowa na kuwa kona, inachongwa, haina manufaa


DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
KADI Dk 90 Mobi analambwa kadi ya njano 
GOOOOOOOOOOO Dk 89 Nonga anaunganisha vizuri mpira wa faulo na kumshinda Manula 
Dk SUB Dk 87 Simba wanamtoa Mavugo aliyeingia na nafasi yake inachukuliwa na Bukaba kuongeza ulinzi 


KADI Dk 84, Juuko analambwa kadi ya pili ya njano na kuwa NYEKUDNU
Dk 84, Kichuya anaachia mkwaju wa adhabu lakini Massawe anazidi kuonyesha yuko vizuri
Dk 83, Simba wanapaswa kuwa makini kwa kuwa MWadui wanaonekana wako kwenye shepu ya kusawazisha
Dk 80 shuti jingine kali karibu na lango la Simba, goal kick
Dk 77, kipa anapangua shuti la Mavugo ilikuwa karibu kabisa
KADI Dk 75, Awesu analambwa kadi ya njano kwa kujiangusha
Dk 73 Awesu anaingia vizuri katika eneo la 18 lakini anajiangusha na mwamuzia namuambia acha ujanja
GOOOOOOOOOOOO Dk 71, kwa mkwaju wa penalti Okwi anaandika bao la pili la Simba, bao la kwaza kwake la mkoani


KADI DK 70 Mgeveke anainuka na kulambwa kadi ya njano
PENAAAAAT Dk 67, Mgeveke anamuangusha Okwi ndani ya 18, wote wawili wako chini
Dk 65, piganikupige kwenye lango la Mwadui lakini Mobi anaondosha
Dk 64, Massawe anafanya kazi ya ziada na kuokoa, inakuwa ni kona
SUB Dk 64 Nicholas Gyan anaingia kuchukua nafasi ya Ndemla
KADI Dk 63 Kipa Massawe, analambwa kadi ya njano baada ya kuda nje ya 18
KADI Dk 61, Juuko analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Sheva au Miraji
GOOOOOOOOO Dk 59 Luhende anafunga bao safi kabisa kwa mkwaju wa adhabu



Dk 58, MWadui FC wanapata faulo nje kidogo ya 18 ya Simba, ni sehemu mbaya hii
Dk 54, MWadui FC wanaonekana kuizidi Simba katika eneo la katikati ya uwanja
Dk 50 Mwadui FC wanaendelea kushambulia kwa kasi, wanapata kona, inachongwa na Awesu, ilikuwa hatari, lakini Juuko anaokoa unakuwa kurushwa
Dk 47, Mwadui wanaonekana wameanza vizuri wakiongozwa na Awesu wametawala eneo la katikati ya uwanja
Dk 45 mpira umeanza kwa kasi, MWadui wanaonekana wanataka kupata bao la kusawazisha



MAPUMZIKO
DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 45, Kichuya anaachia mkwaju mkali kabisa, kipa anadaka
Dk 43, mwamuzi amesimamisha mpira ili wapate mapumziko mafupi ya maji
Dk 41, nje ya 18, Awadhi Juma anaachia mkwaju mkali kabisa, unapita juu kidogo ya lango la Simba
Dk 38 Simba wanapata kona nyingine, inachingwa vizuri kabisa lakini goal kick
Dk 36 Okwi anageuka vizuri, anapiga chenga na kuachia mkwaju maridadi, lakini anaokoa vziuri kabisa
Dk 32 Zimbwe anatoa boko, Miraji yeye na kipa Manula, anaokoa
Dk 31, mpira wa juu kwenye lango la Simba, anaruka juu Manula, goal kick
SUB Dk 29 Mavugo anaingia kuchukua nafasi ya Bocco aliyeumia


KADI Dk 27, Zimbwe analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 26, Mwadui FC wanaonekana kuwa na haraka maana wanapoteza pasi nyingi sana
Dk 22, krosi safi ya Ndemla katikati ya lango mpira unapita bila mwenyewe, mabeki na washambuliaji wanaukosa
Dk 21, mpira safi wa kona wa Ndemla, Kotei anauwahi lakini Mobi anaondosha vizuri kabisa


Dk 20, kipa Massawe anafanya kazi nyingine ya ziada kupangua shuti la Ndemla na kuwa kona
Dk 19, Kichuya anapiga kona fupi kwa Kapombe lakini Luhende anawahi na kuondosha
Dk 18, Okwi akitokea kidogo anaachia krosi lakini beki Mwadui anatoa na kuwa kona
Dk 17, Zimbwe anaingia vizuri pembeni, anaachia krosi lakini kipa Massawe anawahi na kudaka
Dk 15, Kichuya anaachia mkwaju wa kuzungusha, kipa Masawa anadaka vizuri kabisa
Dk 14, Okwi anamtoka Mobi lakini anatoa inakuwa kona, inachongwa, inaokolewa
Dk 12, inachongwa kona hapa, Luhenda anaondosha vizuri kabisa


Dk 11 Kapombe anaingia vizuri, anaachia mkwaju mkali kabisa, kipa anafanya kazi ya ziada anapangua na kuwa kona
GOOOOOOO Dk 9, Bocco anauwahi mpira na kupiga kichwa safi, anaandika bao la kwanza
Dk 7 sasa, bado mpira haujachangamka sana na inaonekana MWadui wanacheza zaidi upande wa lango lao
Dk 5, Simba wanaingia vizuri, pasi nzuri ya Ndemla lakini mpira unampita, MWadui FC wanaokoa
Dk 3, Mwadui FC nao wanafika katika lango la Simba lakini mpira mrefu wa Luhende unakosa mwenyewe
Dk 1, mechi imeanza na Simba wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Mwadui FC, wako makini
 
Chanzo: bin zuber

MKURUGENZI IMARA SACCOS AJITOSA KUGOMBEA URAIS,KESHO KUTANGAZA NIA

BONIPHACE NDENGO



NA AHMAD NANDONDE,



MUSOMA.
MKURUGENZI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO MKOANI MARA (IMARA SACCOS) BW. BONIFACE NDENGO KESHO ANATARAJIA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UCHAGUZI MKUU UNAOTARAJI KUFANYIKA MWEZI OCT. MWAKA HUU.

BW. BONIFACE NDENGO AMESEMA KUWA HATUA YAKE YA KUTAKA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS INAKUJA KUFUATIA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA KIMAISHA, UMASKINI ULIOKITHIRI KATIKA JAMII PAMOJA NA UKOSEFU WA AJIRA HUSUSANI KWA VIJANA NDIYO SABABU KUBWA INAYOPELEKEA YEYE KUCHUKUA UAMUZI HUO.

NDENGO AMEONGEZA KUTOKANA NA KUWAPO KWA WATOTO WAISHIO NA KUSOMA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, WAKULIMA KUDHULUMIWA HAKI ZAO, WAZEE WASTAAFU KUTOPATIWA MAFAO YAO KWA WAKATI, PAMOJA NA UKOSEFU WA HUDUMA BORA YA AFYA NI WAZI KUWA IPO HAJA YA YEYE KUWANIA NAFASI HIYO ILI KUISAIDIA JAMII YA WATANZANIA KUONDOKANA NA TATIZO HILO LINALOIKABILI TANZANIA TOKA ILIPOPATA UHURU WAKE KWA ZAIDI YA MIAKA HAMSINI HIVI SASA.

BW. NDENGO AMBAYE AMEBOBEA KATIKA MASUALA YA UCHUMI NA BIASHARA AMESEMA ANAUCHUKIA UMASIKINI ULIOKITHIRI HAPA NCHINI NA ENDAPO ATAFANIKIWA KUINGIA IKULU KITU CHA KWANZA ATAKACHOKIFANYA NI KUHAKIKISHA ANAIFANYA TANZANIA KUWA KITUO KIKUBWA NA BORA CHA BIASHARA KIMATAIFA NA UTALII BARANI AFRIKA ILI KUONGEZA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA KWANI KAMWE HAONI SABABU YA KUA NA TANZANIA YENYE AMANI AMBAYO WATU WAKE HAWANA AJIRA.

KIJANA HUYO MJASIRIA MALI MWENYE NIA YA DHATI YA KULIKOMBOA TAIFA KATIKA HALI YA UMASIKINI KESHO ANATARAJIA KUTANGAZA NIA YAKE YA KUMRITHI RAIS WA SASA DK. JAKAYA KIKWETE KATIKA VIWANJA VYA MARA CONFERENCE HALL (MCC) SAA NANE MCHANA KABLA YA KUELEKEA MJINI DODOMA SIKU INAYOFUATA AMBAPO SIKU YA JUMANNE ANATARAJI KUCHUKUA FOMU, HUKU AKIWAOMBA WANANCHI KUMIMINIKA KWA WINGI KATIKA MKUTANO WAKE KWAAJILI YA KUMSIKILIZA.



MWISHOO.

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK