`

Home » » MKURUGENZI IMARA SACCOS AJITOSA KUGOMBEA URAIS,KESHO KUTANGAZA NIA

MKURUGENZI IMARA SACCOS AJITOSA KUGOMBEA URAIS,KESHO KUTANGAZA NIA

BONIPHACE NDENGO



NA AHMAD NANDONDE,



MUSOMA.
MKURUGENZI WA CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO MKOANI MARA (IMARA SACCOS) BW. BONIFACE NDENGO KESHO ANATARAJIA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UCHAGUZI MKUU UNAOTARAJI KUFANYIKA MWEZI OCT. MWAKA HUU.

BW. BONIFACE NDENGO AMESEMA KUWA HATUA YAKE YA KUTAKA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA URAIS INAKUJA KUFUATIA CHANGAMOTO MBALIMBALI ZA KIMAISHA, UMASKINI ULIOKITHIRI KATIKA JAMII PAMOJA NA UKOSEFU WA AJIRA HUSUSANI KWA VIJANA NDIYO SABABU KUBWA INAYOPELEKEA YEYE KUCHUKUA UAMUZI HUO.

NDENGO AMEONGEZA KUTOKANA NA KUWAPO KWA WATOTO WAISHIO NA KUSOMA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU, WAKULIMA KUDHULUMIWA HAKI ZAO, WAZEE WASTAAFU KUTOPATIWA MAFAO YAO KWA WAKATI, PAMOJA NA UKOSEFU WA HUDUMA BORA YA AFYA NI WAZI KUWA IPO HAJA YA YEYE KUWANIA NAFASI HIYO ILI KUISAIDIA JAMII YA WATANZANIA KUONDOKANA NA TATIZO HILO LINALOIKABILI TANZANIA TOKA ILIPOPATA UHURU WAKE KWA ZAIDI YA MIAKA HAMSINI HIVI SASA.

BW. NDENGO AMBAYE AMEBOBEA KATIKA MASUALA YA UCHUMI NA BIASHARA AMESEMA ANAUCHUKIA UMASIKINI ULIOKITHIRI HAPA NCHINI NA ENDAPO ATAFANIKIWA KUINGIA IKULU KITU CHA KWANZA ATAKACHOKIFANYA NI KUHAKIKISHA ANAIFANYA TANZANIA KUWA KITUO KIKUBWA NA BORA CHA BIASHARA KIMATAIFA NA UTALII BARANI AFRIKA ILI KUONGEZA FURSA ZA AJIRA KWA VIJANA KWANI KAMWE HAONI SABABU YA KUA NA TANZANIA YENYE AMANI AMBAYO WATU WAKE HAWANA AJIRA.

KIJANA HUYO MJASIRIA MALI MWENYE NIA YA DHATI YA KULIKOMBOA TAIFA KATIKA HALI YA UMASIKINI KESHO ANATARAJIA KUTANGAZA NIA YAKE YA KUMRITHI RAIS WA SASA DK. JAKAYA KIKWETE KATIKA VIWANJA VYA MARA CONFERENCE HALL (MCC) SAA NANE MCHANA KABLA YA KUELEKEA MJINI DODOMA SIKU INAYOFUATA AMBAPO SIKU YA JUMANNE ANATARAJI KUCHUKUA FOMU, HUKU AKIWAOMBA WANANCHI KUMIMINIKA KWA WINGI KATIKA MKUTANO WAKE KWAAJILI YA KUMSIKILIZA.



MWISHOO.

1 comments:

  1. Tuko pamoja kwa kila hatua......@kila mmoja aplay part yake kumsapot...tujiandikishe kwa wingi

    ReplyDelete

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK