`

Home » » AJALI YA MOTO MTO MARA YAUA WATOTO WAWILI

AJALI YA MOTO MTO MARA YAUA WATOTO WAWILI



JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

JESHI LA POLISI TANZANIA

mso16A58

                                
TAARIFA KWA WAANDISHI WA HABARI – 16.03.2015
AJALI YA MOTO NA KUSABABISHA VIFO NA MAJERUHI:

Ndugu Waandishi wa habari; Mnamo tarehe 15.03.2015 majira ya 11:00hrs, huko maeneo ya kijiji cha Buswahili, Kata ya Buswahili, Tarafa ya Kiagata, Wilaya ya Butiama, Mkoa wa Mara. Kandokando ya Mto Mara uliwaka Moto katika matete yaliyokauka na kuenea eneo kubwa.

Katika tukio hilo baadhi ya watu waliokuwa katika shughuli zao waliathiriwa na kusababisha vifo vya watu wawili wanaofahamika kwa majina ya:-  1. KIRARYO S/O MARWA, miaka 14yrs, mwanafunzi wa shule ya msingi Buswahili, 2.TARANGWA S/O ELIAS, miaka 11yrs, mwanafunzi wa shule ya Msingi Buswahili ambaye alifariki akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara.

Aidha katika tukio hili watu watatu walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao ambao ni;- 1. GHATI W/O CHACHA, miaka 40yrs, mkazi wa Buswahili aliyekuwa anapata matibabu katika Hospitali ya Kongoto na ameruhisiwa na hali yake inaendelea vizuri 2. LISO S/O MAGABE, miaka 16yrs, mwanafunzi wa shule ya Msingi Buswahili, 3. MAGWAIGA S/O ZAKARIA, miaka 14yrs, mwanafunzi wa shule ya Msingi Buswahili.

Wavuvi wa kijiji cha Kongoto waliwasha moto huo majira ya 11:00hrs  kwa ajili ya kuwawezesha kusafisha eneo la kuvulia samaki na ndipo moto ulisambaa eneo kubwa na kufika eneo ambalo walikuwepo marehemu pamoja na majeruhi ambao nao walikuwa wanatafuta eneo la kuvulia samaki na kuwazunguka na wakashindwa kujiokoa na kupata madhara hayo.

Moto huo uliokuwa unasambaa kwa kasi kuelekea katika makazi ya watu ulizimwa iliusielekee katika makazi ya watu kwa ushirikiano wa Askari wa Jeshi la Polisi, Wananchi wa eneo hilo na Askari wa Kikosi cha Zimamoto cha Manispaa ya Musoma Mjini.

Mwili wa Marehemu KIRARYO S/O MARWA umekwisha kabidhiwa kwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi na Mwili wa TARANGWA S/O ELIAS umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara na Majeruhi wawili wamelazwa Hospitalini hapo wakiendelea na Matibabu. Hakuna mtu yeyote anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi Kuhusiana na tukio hilo.




WITO.
 kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, anatoa wito kwa wazazi kuwa makini na watoto wao pindi wanapotoka majumbani kwenda kucheza au katika shughuli zingine ili kuepusha madhara yanayoweza kuwapata na kusababisha vifo au hata ulemavu kwao, Pia anawataka wavuvi kuwa makini wanapochoma moto kwa ajili ya shughuli zao za uvuvi ili kuepusha madhara yasababishwayo na moto.



          PHILIP ALEX KALANGI- ACP.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MARA-MUSOMA.


0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK