`

Home » » WAZIRI MAGHEMBE AZINDUA MIRADI YA MAJI SERENGETI NI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI

WAZIRI MAGHEMBE AZINDUA MIRADI YA MAJI SERENGETI NI KATIKA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI








SERENGETI.





WAZIRI WA MAJI BW. JUMANNE MAGHEMBE JANA AMEWEKA MAWE YA MSINGI KATIKA MIRADI MIWILI YA MAJI ILIYOPO KATIKA KATA ZA NYAGASENSE, RUNG'ABURE PAMOJA NA KUTEMBELEA MRADI WA UJENZI WA CHUJIO KUBWA LILILOPO KARIBU NA BWAWA LA MACHIRA MJINI MUGUMU SERENGETI.







AKIZUNGUMZA NA WANANCHI HAO WAZIRI MAGHEMBE AMESEMA KWA KUTAMBUA UKUBWA WA TATIZO LINALOWAKUMBA HUSUSAN AKINA MAMA NDIYO MAANA SERIKALI IKAHAKIKISHA INAWEKA NGUVU ZAKE NYINGI ILI KUHAKIKISHA INAZINDUA MIRADI HIYO MIWILI ILIYOKUWA KATIKA UJENZI HUKU MINGNIE IKWA KATIKA HATUA ZA MWISHO NA HIVYO KUPUNGUZA TATIZO HILO NA HATA PENGINE KULIONDOA KABISA.





AIDHA WAZIRI MAGHEMBE AMEONESHA KURIRIDHISHWA KWAKE NA KASI INAYOFANYWA NA WAKANDARASI WANAOJENGA MRADI WA CHUJIO KUBWA LITAKALOKUWA LIKICHUJA NA KUWEKWA DAWA MAJI KUTOKA BWAWA LA MCHIRA, WAKITARAJIA PIA KUANZA AWAMU YA KWANZA YA UJENZI WA TENKI KUBWA LA MAJI LITAKALOJENGWA KATIKA BWAWA LA MACHIRA.





AMEONGEZA KUWA KATIKA AWAMU YA PILI ITAONGEZA UWEZO WA MAJI ILI IWEZE KUWAFIKIA WANANCHI WA MUGUMU KWA UHAKIKA, KUONGEZA MAMLAKA ZA MAJI KUSAIDIA KATIKA UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA HATA KUSAIDIA MJI HUO HUSUSAN KATIKA SUALA ZIMA LA UTALII.





NAYE MWAKILISHI WA MKURUGENZI WA MAJI WILAYANI SERENGETI AMBAYE PIA NI MKANDARASI WA MAJI WILAYANI HUMO BW. MARWA MURAZA AMEWAOMBA WANANCHI KUHAKIKISHA WANAVITUNZA VYANZO VYA MAJI MIUNDOMBINU YA MAJI IKIWA NI PAMOJA NA KUTUNZA MAZINGIRA ILI KUHAKIKISHA MIRADI HIYO YA MAJI ILIYOZINDULIWA INAKUWA ENDELEVU NA KULETA MANUFAA KWA JAMII HUSIKA.





ZIARA YA UWEKAJI WA MAWE YA MSINGI NA UKAGUZI WA MIRADI YA MAJI INAFANYIKA WAKATI DUNIA IKIWA KATIKA WIKI YA MAJI ILIYOANZA TAREHE 16 MACH NA KUZINDULIWA NA WAZIRI WA MAJI BW. JUMANNE MAGHEMBE NA KUTARAJI KUFIKIA TAMATI MACH 22 AMBAPO RAIS JAKAYA KIKWETE, MKOA WA MARA MWAKA HUU UMEPEWA HESHIMA YA KUWA MWENYEJI KATIKA MAADHIMISHO HAYA YALIYOBEBA KAULIMBIU ISEMAYO "MAJI KWA MAENDELEO ENDELEVU"






0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK