`

Home » » AFRIKA KUSINI YAENDELEA NA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MZEE MADIBA

AFRIKA KUSINI YAENDELEA NA MAOMBOLEZO YA KIFO CHA MZEE MADIBA

Afrika Kusini ambayo imo katika maombolezi  imeanza jana Jumamosi matayarisho ya kuwapokea viongozi mbali mbali duniani kwa ajili  ya mazishi ya aliyepambana dhidi  ya  utawala  wa kibaguzi Nelson Mandela aliyefariki siku ya Alhamisi akiwa na umri wa miaka 95. 

Huku hayo yakiarifiwa kwa mara ya kwanza hapo jana familia yake kupitia msemaji wao Temba Matanzima imezungumzia kifo cha mzee Madiba, na kusema kwamba wamepokea kifo hicho kwa masikitiko makubwa.

Katika sehemu tofauti nchini Afrika kusini raia wa nchi hiyo wamekusanyika pamoja ,katika  makundi madogo na makubwa wakiomboleza na kusherekea maisha ya Mandela ambaye alifungwa na  baadaye  kuwa rais  wa  kwanza  mweusi  nchini  humo  na kuiweka nchi hiyo na kuwa kiashirio cha matumaini na uhuru.
Mzee Nelson Mandela atazikwa siku ya Jumapili katika kijiji cha Qunu mahali alikokulia.

Wakati huo  huo  ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa  rais Barrack Obama na mkewe Michelle Obama watahudhuria mazishi ya Mzee Mandela, wakiwa pamoja na marais wa zamani George W. Bush na mkewe Laura Bush, Bill Clinton na  mkewe  Hillary Clinton, pamoja na Jimmy Carter.

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK