`

Home » » MALINZI MGENI RASM MASHINDANO YA KAWAMBWA CUP

MALINZI MGENI RASM MASHINDANO YA KAWAMBWA CUP



 Na Ahmad Nandonde,

Bagamoyo.

Rais wa TFF jamal malinzi leo anataraji kuwaq mgenio rasmi katika fainali za mashindano ya kawambwa cup itakayofanyika katika uwanja wa mwanakalenge mjini bagamoyo mkoani pwani.


Akuzungumza na blog ya jicho la mdadisi afisa habari wa mashindano hayo masau bwire alisema kuwa fainali hiyo itakayoanza majira ya saa kumi kamili za jioni inatarajiwa itazikutanisha timu za mwambao fc na maji coast zote kutoka mjini bagamoyo.


Masau aliongeza kuwa katika fainali hiyo rais mpya wa tff jamal malinzi atakabidhi zawadi kwa washindi wa michuano hiyo ambapo mshindi wa kwanza atajinyakulia kikombe, jezi seti mbili, mipira miwili na fedha taslimu shilingi 400,000 mshindi wa pili atajinyakulia jezi seti mbili, mipira miwili fedha taslimu shilingi lakini 300,000 huku mshindi wa tatu akijipatia jezi seti moja mpira mmoja na fedha taslimu shilingi 200,000.


Lakini mbali na zawadi hizo kutolewa kwa mshindi wa wakwanza wapili na watatu pia kutakuwa na zawadi nyingine kwa timu yenye nidhamu ambayo itajinyakulia shilingi laki 100,000 ikiwa ni pamoja na kutolewa tuzo maalumu kwa mchezaji bora, mfungaji bora na kipa bora na mwamuzi bora wa mashindano hayo.


Ili kuongeza chachu katika burudani fainali hizo za kawambwa cup itatanguliwa na michezo mingine ambapo kutakuwa na mpira wa miguu wa wanawake utakaozikutanisha timu ya bagamoyo queen dhidi ya na vijana kombaini michezo mingine ni pamoja na kufukuza kuku kna kuvuta kamba ambapo pia washindi watajinyakulia zawadi.


Mashindano hayo ya kawambwa cup yalianzia katika ngazi ya kata kwa kuzishirikisha timu 72 kutoka kata zote zilizopo jimbo la bagamoyo ambazo zilifanikiwa kuingia katika hatua ya timu 16.

Viongozi mbalimbali wa michezo mkoani pwani na wailayani bagamoyo na wapenzi na wadau wa soka kutoka sehemu mbalimbali wanataraji kuhuidhuria katika mashindano hayo yatakayopigwa jioni ya leo.

Mwisho………….

                                            Jamal Malinzi rais TFF pichani
                                 

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK