Ni hayati mzee Jomo Kenyata wa Kenya baba mzazi wa rais wasasa wa kenya uhuru kenyata ambae mara kwa mara aliwaacha hoi na kuwavunja mbavu watu waliokuwa wakisikiliza hotuba zake.
Katika tukio moja Mzee Kenyata aliwaonya watu wanaosema kwamba ang'atuke katika siasa kwa sababu umri wake umekuwa umekwenda mno (amezeeka).
Mzee Kenyata alisema maneno haya "Ati iko mutu nasema mimi nimezeeka ? ati nimezeeka? Hebu muulizeni mama Ngina (mkewe) kama mimi nimezeeka" baada ya maneno hayo yaliyoshangiliwa sana na wananchi, ghafla mtu mmoja akaropoka kwa sauti kuu "Sawa mzee ongoza sisi tuko nyuma yako..."
Mzee Kenyata akadakia "Ati unaona hii mutu ya Mombasa! muko nyuma yangu nataka kunifanya nini? sema tuko bega kwa bega
"Ebooh..."
0 comments:
Post a Comment