`

Home » » SERIKALI MKOANI MARA YAAHIDIKUSIMAMIAA SER

SERIKALI MKOANI MARA YAAHIDIKUSIMAMIAA SER

MUSOMA.

SERIKALI MKOANI MARA IMESEMA ITAENDELEA KUSIMAMIA SERA NA UTARATIBU ULIOWEKWA KWAAJILI YA KUPAMBANA NA CHANGAAMOTO MBALIMBALI ZINAZOWAKABILI WAJASIRIAMALI WA MKOA WA HUO.

HAYO YAMESEMWA MJINI MUSOMA NA MKUU WA MKOA WA MARA BW JOHN GABRIEL TUPPA,KATIKA HOTUBA YAKE AMBAYO IMESOMWA NA MKUU WA WILAYA YA MUSOMA BW JACKSON MSOME KATIKA KONGAMANO LA WAJASIRIAMALI LILILOANDALIWA NA TAASISI ISIYO YA KISERIAKLI YA NYANGOTO DEVELOPMENT GROUP YA MKOA WA MARA.

KATIKA HOTUBA HIYO MKUU WA MKOA WA MARA AMESEMA KUWA KUMEKUWEPO NA CHANGAMOTO MBALIMBALI AMBAZO ZINAWAKABILI WAJASIRIAMALI MKOANI HUMO AMBAPO SERIKALI YA MKOA ITAENDELEA KUSIMAMIA SERA NA UTARATIBU HUO  KATIKA KUPAMBANA NA CHANGAMOTO HIZO ILI KUWEZESHA KUNDI HILO KATIKA JAMII LINAPATA MITAJI KWA RIBA NAFUU NA HIVYO KUWEZESHA KUPAMBANA NA UMASIKINI.

HATA HIVYO MKUU WA MKOA WA MARA,AMEWATAKA WAJASIRIAMALI HAO PIA KUJIUNGA NA MFUKO WA AFYA YA JAMII CHF  KAMA NJIA YA KUIMARISHA AFYA ZAO NA FAMILIA ZAO.

NAYE KATIBU WA TAASISI YA NYANGOTO DEVELOPMENT GROUP AMBAYE PIA NI MJUMBE WA BARAZA LA UWT TAIFA KUTOKA MKOANI MARA BI AGNESS METHEW,AMBAYE AMECHANGIA SHILINGI MILIONI KUMI KATIKA MFUKO WA KUWASAIDIA WAJASIRIAMALI,AMESEMA LENGO LA KUWAKUTANISHA WAJASIRIAMALI HAO NI KUTAKA KUTAMBUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI NA KUTAZAMA JINSI YA KUZITATUA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI MKOANI HAPA.

KATIKA KONGAMANO HILO ZAIDI YA WAJASIRIAMALI 1000 WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA TOFAUTI WAMEJITOKEZA AMBAPO KIASI CHA SHILINGI MILIONI KUMI NA SITA ZILIPATIKANA KATIKA HARAMBEE ILIYOFANYIKA SANJARI NA KONGAMANO HILO.

,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK