MUSOMA:
WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO AMESEMA WATANZANIA WANAPASWA KUKUBALIANA NA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME ILIYOTANGAZWA NA EWURA HIVI KARIBUNI KULIKO SABABISHWA NA MAMBO MBALIMBALI IKIWEMO KULAZIMIKA KUNUNUA UMEME KWA GHARAMA KUTOKA KWA WAZALISHAJI WA DHARURA (EMERGENCY POWER PRODUCERS).
AMESEMA HALI YA UZALISHAJI WA UMEME WA NDANI KWA KUTUMIA MAJI KATIKA MABWAWA YA KUZALISHIA UMEME BADO SIO NZURI NA HIVYO TANESCO ITAENDELEA KUNUNUA UMEME KUTOKA KWA WAZALISHAJI WA DHARURA KWA KIPINDI HIKI AMBACHO SERIKALI KUPITIA WIZARA YA NISHATI NA MADINI INAFANYA JITIHADA KUBWA YA UZALISHAJI WA UMEME WA GESI.
WAZIRI MUHONGO AMESEMA SULUHISHO LA KUPATA UNAFUU WA GHARAMA ZA UMEME NI PALE UTAKAPOANZA UZALISHAJI WA UMEME WA GESI AMBAO UTAKUWA NI NAFUU ZAIDI LAKINI KWA SASA WATANZANIA INABIDI WAKUBALIANE NA ONGEZEKO HILO LILILOTANGAZWA.
KATIKA MAZUNGUMZO YAKE NA VIJANA WA MJI WA MUSOMA JUU YA UCHUMI NA MAENDELEO PAMOJA NA HALI YA UMEME NCHINI,PROFESA MUHONGO ALISEMA LICHA YA KUTANGAZWA KWA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME BADO UMEME WA TANZANIA UPO CHINI TOFAUTI NA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI KUNAKOPELEKEA NCHI NYINGINE KULALAMIKA KUTOKANA NA MASHIRIKIANO YA KIBIASHARA YA NCHI HIZO KATIKA JUMUIYA.
AMESEMA TANZANIA IMEFANYA UNGEZEKO LA UMEME KUTOKA SENTI 12 HADI 16.2 KWA UNIT AMBAPO KENYA INAUZA UMEME SENTI 18 KWA UNIT HUKU UGANDA IKIUZA UMEME WAKE WA SENT 19 KWA UNIT HIVYO BADO UMEME WA TANZANIA UPO CHINI NA WATANZANIA WAPOKEE ONGEZEKO HILO LA MUDA.
ALIDAI TANESCO WALIOMBA KUIDHINISHWA KWA KANUNI YA KUREKEBISHA BEI YA UMEME KULINGANA NA MABADILIKO YA BEI ZA MAFUTA, MFUMUKO WA BEI NA MABADILIKO YA THAMANI YA SHILINGI YA KITANZANIA NA KUSEMA ONGEZEKO HILO LINGEANZA TANGU MWAKA JANA LAKINI ILISHITISHWA KUTOKANA NA KUPUNGUZA BEI YA KUUNGANISHIWA UMEME ILI KUPATA WATEJA WENGI WATAKAOWEZA KUCHANGIA UMEME.
Mwisho......
Home »
» WAZIRI MUHONGO AWATAKA WATANZANIA KUKUBALIANA NA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME.
0 comments:
Post a Comment