`

Home » » ZAIDI YA SHILINGI BILION 27.7 ZAPITISHWA KIKAO CHA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA HALMASHAURI YA MUSOMA.

ZAIDI YA SHILINGI BILION 27.7 ZAPITISHWA KIKAO CHA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA HALMASHAURI YA MUSOMA.

Na Ahmad Nandonde,

Musoma.


Zaidi ya shilingi billion ishirini na saba nukta saba zimepitishwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2014 / 2015 ya halmashauri ya musoma kwaajili ya mishahara, maendeleo na matumizi  mengineyo.

Hayo yemesemwa jana na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya musoma bi. Fidelica myovela katika kikao cha bajeti cha baraza la madiwani wa halmashauri ya musoma kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa halimashauri hiyo.


Bi. Myovella amesema kuwa halmashauri hiyo imeidhinisha zaidi ya shilingi bill. 15.7 ambayo ni sawa na asilimia 56.91, matumizi mengineyo ambayo ni zaidi ya shilingi billion nne nukta 2 ambayo ni sawa na asilimia 15.37 pamoja na matumizi ya mengineyo ambayo ni zaidi ya billion 7 nukta 6 sawa na asilimia 27.72.


Amesema mpango wa bajeti na mapato ya matumizi ya kawaida maendeleo ya mwaka fedha 2014 / 2015 umeandaliwa kwa kuzingatia ilani ya chama tawala mwaka 2010, mpango mkakati wa miaka mitano ya halmashauri ya wilaya, mpango wa kukuza na kupunguza umaskini mkukuta awamu ya pili na mkakati wa kitaifa wa kilimo kwanza.

Mpango mwingine ni ahadi na maagizo ya serikali, malengo ya millenia yaliyolengwa kufikia mwaka 2015, vipaumbele vya kiwilaya, kimkoa na kitaifa,sera na miongozo mbali mbali ya kisekta na kiprogramu pamoja na mpango wa tekeleza sasa kwa matokeo makubwa big results now (brn).

Myovela ameongeza kuwa bajeti hiyo inayozingatia celling ya halmashauri imeandaa maombi maalumu ya zaidi ya shilingi billion 14 nukta 6 kwaajili ya ujenzi wa mradi wa umwagiliaji kataryo, ukarabati wa mradi wa umwagiliaji kijiji cha maneke, ujenzi wa soko la dagaa na mazao mengineyo kijijini busekela,

Maombi mengine ni ya ujenzi wa jengo la utawala makao makuu ya halmashauri murangi, ujenzi wa soko la mazao kijiji cha suguti, ununuzi wa magari mawili ya moja la mkurugenzi mtendaji wa wilaya na lingine la idara ya mipango takwimu na ufuatiliaji pamoja na ununuzi wa gari la wagonjwa (ambulance) katika kituo cha afya cha murangi.

Mwisho……

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK