Na Ahmad Nandonde,
Musoma.
JUMLA ya watoto wapatao
ishirini waliofaulu mtihani wa darasa la saba na kushindwa kwenda shule kwa
ukosefu wa ada katika kata ya kyenyari wilayani butiama wanataraji kusomeshwa
bure katika elimu ya sekondari.
Hayo yalisemwa jana na
mjumbe wa mkutano mkuu kata ya kenyari ambaye pia ni mjumbe huyo wa halmashauri
kuu ccm kwa upande wa vijana (uvccm) wilayani butiama bw. Mgingi Muhochi
alipokuwa akiwahutubia wananchi wa kijiji cha mwibagi kata ya kyenyari wilayani
butiama.
Bw. Muhochi alisema ili
kuendana na mpango wa serikali wa matokeo makubwa sasa (BRN) hivyo kuamua
kuchukua jukumu la kuwasaidia watoto waliofaulu toka katika kitongoji cha
Nyakiswa watano, Mwibagi sita, Nyamikoma tisa ambao jumla yake itakuwa ni
watoto ishirini.
“Nimejaribu kushirikiana na
watu kupitia ilani ya chama cha mapinduzi nilileta barua ili niweze kupata
watoto nitakaoweza kuwasidia kupata elimu ya sekondari katika sekondari ya
kyenyari kwani hata mimi nimepitia katika mazingira magumu” alisema….
“Katika kata hii kuna jumla
ya watoto mia moja waliofaulu lakini kwa uwezo nilionao ninawaomba viongozi wa
vijiji kusaidia kupatikana watoto ishirini kutoka kitongoji cha nyakiswa
watano, mwibagi sita, nyamikoma tisa ambao jumla yao itakuwa ni watoto
ishirini” aliongeza…
Muhochi ameongeza kuwa hivi
sasa tayari ameshatuma barua kwa viongozi wa vijiji ili kuwapata watoto hao
watakaoanza masomo katika sekondari ya kyenyari na hivyo kuwahimiza kuwa kabla
ya feb 2 watoto hao wawe wameshapatikana.
“Mpaka feb. 2 mwaka huu
naomba niwe nimeshapata majina ya watoto hao katika kata hii ambao
watapatiwa elimu shuleni hapo ili
waweze kupata elimu itakayowasaidia katika maisha yao”
Awali bw. Muhochi alimtupia lawama mtendaji wa
kata ya kyenyari bw. Alfred Kitambala na kusema kuwa mtendaji huyo amekuwa ni
mzigo kwa wananchi wa kata hiyo kwa kudidimiza shughuli za kimaendeleo kwa
kutokamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule ya msingi mwibagi na
maabara ya shule ya sekondari ya kyenyari.
Hata hivyo mjumbe huyo wa
halmashauri kuu ccm kwa upande wa vijana (uvccm) wilayani butiama amemuomba
mkurugenzi wa wilaya hiyo kumuondoa mtendaji Kitambala katika kata hiyo
kutokana na kutowajibika katika majukumu yake ipasavyo.
“Kutokana na uzembe
unaooneshwa na kiongozi huyu wa kata ninamuomba mkurugenzi wa wilaya amuondoe
mtendaji huyu ambaye ameshindwa kabisa kutekeleza majukumu yake katika kata
yetu” alimalizia………
Mwishooo…..
0 comments:
Post a Comment