WAKATI VIJANA
WENGI WAKITAMANI NA HATA KUJARIBU KUINGIA KATIKA TASNIA YA UDJ..DJ MAARUFU
NCHINI DJ CHOKA AMETANGAZA KUACHANA NA KAZI HIYO RASMI HUKU AKIZITAHJA SABABU
ZA KUACHANA NA KAZI HIYO ZAIDI JICHO LA MDADISI LINAKUPEKULIA HAYO.
Dj maarufu
nchin dj choka ametangaza rasm kuachana na kazi hiyo aliyoitumikia kwa kipindi
kinachokaribia miaka kumi huku akieleza kuwa sababu za kuachana na kazi hiyo
kuwa ni ameona apumzike na kuendelea na kazi inayomuingizia kipato yani blog
yake.
Kazi ya kudj
wasanii ni kazi fulani nzuri lakini ni ngumu sana usipokuwa na hobby nayo,
nimeifanya kazi hii kwa mapenzi yangu mwenyewe yakupenda mziki na sikuwahi
kulalamika mslahi ninayoyapata kwasababu niliifanya kazi hii kwa mapenzi yangu
mwenyewe hata napokuwa jukwaani nilikuwa nafurahia sana.
Lakini kwa kuwa
kazi hii ya kuandika habari na kuonyesha kazi za wasanii wa hapa nchini ndio
inayonilipa vizuri basi naona sina budi kupumzisha kimoja ili niendelee na
kimoja.
Baada ya kupumzisha kazi
yakudj kwenye majukwaa na kuwa dj sasa nitakuwa naendelea na kazi yakuvumbua
vipaji vya wasanii ikiwa ni pamoja na kuendelea kutengeza mix tape zangu kama ilivyoada.
Ameongeza kuwa Msanii
atakayemuhitaji kwa sasa basi ajue itakuwa kazi yakwenda kupiga picha show zake
au kurecord show zake tu pindi atakapokuwa jukwaani.
Mbali na hayo pia amesema
ataendelea kupromoti mziki wa nyumbani na wasanii wake mpaka siku ya mwisho wa
maisha yake.
Lakini mbali ya yote hayo
hakuacha kuwazungumzia madj ambao ndityo kwanza wana malengo ya siku moja kuwa
kama yeye amesema kuwa amefungua pia ukurasa mpya kwa kuwakaribisha dj's under
ground waliopenda sana
kazi hiyo na kukosa wapi kwa kuanzia.
Amesema atakuwa akiwapatia
ushauri ikiwa ni pamoja na kuwafundisha njia za kuwa dj na hata njia za
kuwachezesha wasanii wa hip hop na bongo flava pindi wawapo jukwaani jinsi ya
kucheza nao na hata namna ya kulitawala jukwaani na kusababisha shngwe kwa
mashabiki waliofurika.
Hata hivyo akamalizia kwa
kusema kuwa anawapenda sana
wadau wake wote wa DJCHOKA MUSIC kwani wao yeye aingekuwa hapo alipofikia.
CHOKA KATIKA POZI
0 comments:
Post a Comment