CHEDIELI YOHANE MGONJA (1934-2009) ALIKUWA MWANASIASA WA
TANZANIA ALIZALIWA 31 DESEMBA 1934, VUDEE SAME-MAGHARIBI (WILAYA YA SAME).
ELIMU
NA NYADHIFA ALIZOKUWA NAZO
ALISOMA
SHULE YA MSINGI VUDEE, NA SEKONDARI ILBORU NA TABORA.
1959
---CHUO KIKUU MAKERERE.
1960
---BWANA SHAURI TANGA.
1961
--- MIONGONI MWA WATANGANYIKA SITA WALIOTUNUKIWA ZAWADI KWA KUSHIRIKI KTK
SHINDANO LA UTENZI WA WIMBO WA TAIFA WA TANGANYIKA.
1961
--- 62 CHUO KIKUU CAMBRIDGE UK -- KOZI YA UTAWALA NA DIPLOMASIA. WENGINE KATIKA
KOZI HIYO NI WALIOAPATA KUWA MABALOZI GEORGE NHIGULA,JOHN MALECELA, BERNARD
MULOKOZI, RAPHAEL LUKINDO, AKILI DANIEL.
1962
--- UBALOZI WA TANGANYIKA NEW YORK.
1964
--- KUOMBA KURUDI NYUMBANI KWA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE.
1965
--- KUPIGANIA UBUNGE WILAYA YA PARE VS NAIBU WAZIRI NA KATIBU MWENEZI WA TANU
ELIAS KISENGE.
1965
--- 67 MBUNGE WILAYA YA PARE, WAZIRI WA MAENDELEO NA UTAMADUNI NA HIVYO
KUWEKA REKODI YA KUWA WAZIRI KIJANA
KULIKO WOTE NCHINI.
1967 -- 68 WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAISI ( MAMBO YA NJE ).
WAZIRI
WA KWANZA KUJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT, BAADAYE KUENDELEA NA MAFUNZO YA MGAMBO,
WAZIRI ALIYETOA TAMKO LA SERIKALI YA TANZANIA KUITAMBUA JAMHURI YA WATU WA
BIAFRA.
1968
-- 72 WAZIRI WA ELIMU. MABADILIKO MAKUBWA KATIKA MFUMO WETU WA ELIMU
YALIFANYIKA KIPINDI CHA UONGOZI WAKE.
1972
-- 75 MKUU WA MKOA NA KATIBU WA CHAMA MTWARA. NI UTEUZI PEKEE AMBAO MWALIMU
ALIMJULISHA KABLA HAUJATANGAZWA. ILIKUWA NI KIPINDI CHA MADARAKA MIKOANI NA
VITA YA UKOMBOZI YA MSUMBIJI. MKOA WA MTWARA KUSHIKA NAFASI YA PILI, UKIFUATIA
DAR ES SALAAM, KATIKA KUCHANGIA VITA VYA UKOMBOZI.
1977 -- MKUU WA MKOA NA KATIBU WA CHAMA TABORA.
1977
-- 1980 WAZIRI WA UTAMADUNI, VIJANA, NA MICHEZO. TANZANIA KUKATAA SHINIKIZO LA
MAREKANI KUSUSIA MICHEZO YA OLIMPIC MJINI MOSCOW KATIKA UJUMBE ULIOLETWA NA
MOHAMEDA ALLY WA MAREKANI.
1980
-- 1982 KUSHINDA UBUNGE: KUSHINDA KESI DHIDI YAKE MAHAKAMA KUU ARUSHA NA
KUVULIWA UBUNGE NA MAHAKAMA YA RUFAA TANZANIA.
1984
-- KUTEULIWA NA RAIS KUWA MKUU WA MKOA SHINYANGA.
1985
-- 95 MBUNGE WILAYA YA SAME: VS JONAS MANENTO (85) VS. DR.KIVURUNYA MTERA (90).
ENZI ZA UHAI WAKE MGONJA ALIWAHI KUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA,
TABORA NA MTWARA.
MAREHEMU
MGONJA ALIINGIA KWENYE SIASA MWAKA 1965, AKIWA MBUNGE WA UPARE / SAME NA MWAKA
HUO HUO AKATEULIWA KUWA WAZIRI WA UTAMADUNI, SIASA NA MICHEZO.
MGONJA
ALIKUWA KWENYE SIASA MPAKA MWAKA 1995, AMBAPO WAKATI WOTE ALIKUWA
AKILIWAKILISHA WILAYA YA SAME NA KUFANIKIWA KUONGOZA WIZARA MBALIMBALI KATIKA
SERIKALI YA AWAMU YA KWANZA.
MAFANIKIO YA MGONJA KATIKA WILAYA YAKE YA SAME.
KWA
UPANDE WA ELIMU ALIWEZA KSISITIZA UJENZI WA SHULE ZA MSINGI KATIKA KILA KATA
ILIYOKUMO NDANI YA JIMBO LAKE LA SAME NA NDIO MAANA WAKATI WAKE WASOMI WENGI
WALITOKA KATIKA MIKOA YA UPARENI NA KILIMANJARO KWA UJUMLA.
UJENZI WA MIUNDO MBINU:
WILAYA
YA SAME INA MILIMA MINGI SANA, LAKINI PAMOJA NA MILIMA HIYO WANANCHI WA SAME
CHINI YA UONGOZI WA MAREHEMU MGONJA WALIWEZA KUCHONGA BARA BARA KWENYE
MITEREMKO HIYO MIKALI, KWA KUTUMIA FALSAFA AMBAYO WAPARE WANAITA
"MSARAGAMBO".
KUFUATIA
UCHONGAJKI HUO WA BARA BARA ULIYOFANYWA NA WANANCHI WA SAME VUDEE NDIPO RAIS WA
JAMHURI YA MUUNGANO JULIUS KAMBARAGE NYERERE ALIPOTEMBELEA MAENEO HAYO NA
KUJIONEA KAZI NZURI YA UJENZI WA BARABARA ILIYOFANYWA NA WANANCHI WA SAME VUDEE
NA HIVYO KUWAPACHIKA JINA LA UTANI “WACHINA” WA TANZANIA.
MNAMO
MWAKA 1983 RAIS WA KWANZA WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MWALIMU
J.K.NYERERE ALIMTEUA MGONJA KUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA KABLA YA KUMALIZIKA
ADHABU YAKE.
BAADA
YA MWALIMU KUMTEUA KUWA MKUU WA MKOA WA SHINYANGA MWANASHERIA MKUU KWA WAKATI
ULE MZEE JOSEPH SINDE WARIOBA ALIPOMSHAURI MWALIMU KUWA SUALA HILO LINGELETA
MGOGORO WA KIKATIBA NDANI YA BUNGE NA HIVYO KUPELEKEA WAZIRI MKUU WA WAKATI HUO
MAREHEMU EDWARD MORINGE SOKOINE KUMSHAURI MWALIMU NA KUTENGUA UTEUZI WAKE.
MNAMO
MWAKA 1977 -- 1980 AKIWA KAMA WAZIRI WA UTAMADUNI, VIJANA, NA MICHEZO ALIKATAA
SHINIKIZO LILILOTOLEWA NA MAREKANI KUSUSIA MICHEZO YA OLIMPIC MJINI MOSCOW
KUFUATI UJUMBE ULIOLETWA NA MOHAMEDA ALLY KUTOKA MAREKANI.
MNAMOP
MWAKA 1980 -- 1982 ALISHINDA KESI YAKE ILIYOKUWA IKIENDESHWA KATIKA MAHAKAMA
KUU MJINI ARUSHA IKIWA NI PAMOJA NA
KUSHINDA KITI CHA UBUNGE BAADA YA KUVULIWA UBUNGE.
KUFUATIA
KESI HIYO KABLA MWALIMU NYERERE HAJAONDOKA MADARAKANI ALIMPUNGUZIA MGONJA
ADHABU YAKE NA HIVYO KUGOMBEA TENA UBUNGE WA SAME KATIKA UCHAGUZI ULIOFANYIKA MWAKA
1985, BAADA YA WA JIMBO LA SAME KUMPA USHINDI WA KISHINDO.
HAKUISHIA
HAPO TU KWANI KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 1990, WANANCHI WA SAME, WALIENDELEA
KUMUWEKA TENA BUNGENI KIPENZI CHAO CHEDIELI YOHANE MGONJA "KAGHEMBE"
NA KUDUMU NAFASI HIYO HADI MWAKA 1995 ALIPOAMUA KUACHANA NA MAMBO YA KISIASA.
CHEDIELI
YOHANE MGONJA ALIFARIKI
TAREHE 30 JANUARI 2009, KWA UGONJWA WA KISUKARI NA SHINIKIZO LA DAMU JIJINI DAR
ES SALAAM NA AMEACHA MKE ALIYEJULIKANA KWA JINA LA LILIAN MGONJA NA BADO YUKO
HAI KIJIJINI KWAKE VUDEE SAME MAGHARIBI.
MGONJA
ALIKUWA NI MKAZI WA KIJIJI CHA VUDEE SAME KILIMANJARO.
MWISHO…………………..
0 comments:
Post a Comment