`

Home » » MWEKAHAZINA TASWA AFARIKI DUNIA.NI SULTAN SIKILO.

MWEKAHAZINA TASWA AFARIKI DUNIA.NI SULTAN SIKILO.

MWEKA Hazina wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) na timu ya soka ya chama hicho, Sultan Sikilo amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitli ya Rufaa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kwa masikitiko makubwa Katibu wa TASWA, Amir Mhando amesema kuwa Sikilo alifikishwa hospitali ya Muhimbili, ambako umauti uimfika akitokea hospitali ya Temeke, Dar es Salaam, Alhamisi wiki hii.

“Ndugu yetu aligundulika ana matatizo ya homa ya ini siku ya Alhamisi katika hospitali ya Temeke na akahamishiwa Muhimbili, ambako umauti umemfika,”amesema Mhando.

Mhando amesema msiba wa marehemu upo nyumbani kwa wazazi wake Mbagala Maji Matitu na mazishi yanatarajiwa kufanyika leo Saa 9:00 Alasiri eneo la Kibada, Kigambni, Dar es Salaam.

Wakati wa uhai wake marehemu aliwahi kufanya kazi na kituo cha Times fm wakati huo kikiwa mtaa wa lugoda gerezani,Kher fm, Radio Uhuru Ripota wa michezo Radio Abood na hata wakati mwengine alikuwa akiripoti Radio ambayo ninaifanyia kazi kwa sasa Radio victoria mkoani Mara.

Mungu aiweke mahali pema peponi roho ya marehemu. Amin.


SULTANI SIKILO WAKATI WA UHAI WAKE PICHANI MWENYE T-SHIRT NYEKUNDU AKIONDOLEA KATIKA GHASIA NA MASHABIKI WA YANGA.

JINSI NILIVYOMFAHAMU MAREHEMU SULTAN SIKILO.

Nilimfahamu marehemu Sultan Sikilo kupitia kwa mwandishi mwenzangu Fatma Abdalah Chikawe wakati nikifanya kazi mkoani mtwara na kituo cha Info radio alipokuja kuanzisha chama cha waandishi wa habar za michezo mkoani humo.

Tulikuwa karibu mno na baada ya mimi kuacha kazi mkoani mtwara ndipo aliponishawishi kuingia katika kitu kingine cha radio cha radio kher yeye akiwa kama mhariri mkuu wa kipindi cha michezo wakati huo tulikuwa tukifanya kipindi hicho mimi Mbwana Shomar na marehemu.

kiukweli nitamkumbuka kwani kwa upande wangu ilikuwa ni nadra sana wakati wa kufanya mahojiano ya njia ya simu kufabnya na watu kama akina kocha Julio, Aden rage, kocha Minziro lakini marehemu alikuwa akinambia kijana kaza butui na haukuna haja ya kuogopa unapoandaa kipindi na hii ni kutokana na changamoto walizokuwa nazo watu hao wakati wakufanya nao mahojiano.

Nitamkumbuka sana sikilo kwani mbali na yote hayo lakini alikuwa pia msaada mkubwa kwangu na aliwahi pia kunishawishi kutangaza mipira kwa mfano nakumbuka mchezo kati ya yanga na azam walipofungwa mabao matatu na kutokea fujo na ule wa ashanti na yanga katika uwanja wa taifa wakati huo tulikuwa tukitangaza na radio Abood ya mjini morogoro.

kuna wakati mwingine akiwa nje ya kazi alikuwahi kunipa jukumu la kuripoti matukio kadha wa kadha ya kimichezo na hata kutangaza mpira.na Radio Abood enzi za marehemu julius nyaisanga akiwa mkurugenzi wa chombo hicho.

Binafsi imeniuma sana kwani aliweza kunikutanisha na viongozi mbali mbali wa soka akiwemo Yasin Abdalah, Michael Richard Wambura, na hata Boniface Wambura kwani nakumbuka siku moja wakati tunaingia taifa kutangaza mpira nilikuwa sina kitambulisho maalumu kinachotumiwa na waandishi wa habari kuingia uwanjani, marehemu alinikutanisha na wambura kwaajili ya kupatiwa kitambulisho cha kuingilia uwanjani ambacho hutyolewa na TFF wakati huo.

Lakini mbali na uwezo wake kati uandaaji na utangazaji wa kipindi cha michezo pia alikuwa ni mchezaji wa timu ya taswa kam kiungo wakati na alikuwa mahiri mno katika kulisakata kabumbu.

Nilipokuwa nakuja mkoani mara nilimjuza na yeye alinipa moyo na kuniambia nikaze buti na ipo siku nitafika mbali.

Wakati wa uhai wake marehemu aliwahi kufanya kazi na kituo cha Times fm wakati huo kikiwa mtaa wa lugoda gerezani,Kher fm, Radio Uhuru Ripota wa michezo Radio Abood na hata wakati mwengine alikuwa akiripoti Radio ambayo ninaifanyia kazi kwa sasa Radio victoria mkoani Mara.

Marehumu alikuwa ni kipenzi cha watu, na mcha mungu na pia alikuwa ni mfuasi mzuri wa dini ya kiislamu kwani ilikuwa ni nadra sana kumuona akiacha vipindi vya swala kwani nakumbuka mara kadhaa hata tukiwa uwanjani alikuwa akifanya ibada katika vyumba vya kutangazia mpira.

Mola amlaze mahala pema peponi SULTAN SIKILO. amina.

Mwisho.........



0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK