Na Ahmad Nandonde,
Musoma.
Ili kuhakikisha maboresho ya huduma ya afya kwa watoto
waliochini ya umri wa miaka mitano mradi wa tibu homa unaofadhiliwa na serikali
ya watu wa marekani kwa kushirikiana na wizara ya afya na ustawi wa jamii
imefanya mkutano wake kwa lengo la kujadili tathmini ya utekelezaji wa huduma
hiyo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano mgeni rasmi
katika mkutano huo ambaye pia katibu tawala wa mkoa bw. Benedict Ole Kuyan
amesema kuwa mradi huo umelenga kupunguza vifo vya watoto vinavysababishwa na
magonjwa yanayoambatana na homa kama vile numonia na kuhara na malaria kwa
kuongeza ufanisi wa utambuzi na matibabu sahihi.
Amesema kuwa ili kuhakikisha vifo vinapungua ni wazi kuwa
ipo haja ya kupatikana na ufikiwaji wa wa huduma za afya ya msingi, kuhakikisha
huduma zinaboreshwa kwa watoto waliochini ya umri huo zinakuwa endelevu, ikiwa
nim pamoja na kuishirikisha jamii kuboresha tabia ya kupata kinga na huduma za
afya kila mara na hata mara baada ya mradi huo kumalizika.
Aidha Bw. Kuyan ameongeza kuwa vifo kwa watoto waliochini
ya miaka mitano badi ni tatizo kubwa duniani hususani kwa nchi zilizopo kusini
mwa jangwa la sahara kufuati takwimu ya sensa ya afya ya mwaka 2010 nchini
inaonesha kuwa vifo vya watoto waliochini ya umri wa miaka mitano vimepungua
toka 112 hadi kufikia 81 kati ya watoto 1000 waliozaliwa wakiwa hai.
Amesema kwa kanda ya ziwa idadi ya vifo imepanda kwa vifo
109 kati ya watoto 1000 waliozaliwa wakiwa hai na hii ni kutokana na kutokana
na kushindwa kudhibiti mazalia ya mbu pamoja na maambukizi huku takwimu
zikionesha kuwa mkoa wa mara ukikumbwa na kiasi kikubwa cha maambukizi ya
malaria kinachofikia asilimia 25.
Akizungumza kwa niaba ya mganga mkuu wa mkoa bw. Wilson Winani
mratibu wa malaria mkoani mara bi. Tukaye Lisso amewashukuru wawezeshaji mradi
wa tibu homa na wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa usaidia zoezi zima la
kusaidia uboreshaji wa afya ya watoto waliochini ya umri miaka mitano.
Aidha bi. Lisso amesema
kuwa ili kuenda sanjari na matakwa ya mradi huo hivi sasa wamedhamiria kutoa
elimu kwa wahudumu katika suala zima la utoaji huduma za kiafya ikiwa ni pamoja
na kuwataka wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao hospitalini pindi
wanapogundua dalili za ugonjwa ndani ya masaa 24 ikiwa ni pamoja kuachana na
tabia ya kujitibia wenyewe kabla ya kupatiwa vipimo toka vituo vya afya.
Kwa upande wake mganga mkuu
wa halmashauri ya musoma dk. Genchwele Makenge amesema vifo vya watoto nchini
bado ni changamoto kubwa ingawa serikali kupitia ngazi ya mkoa imeweka mikakati
ya kuhakikisha vifo vya watoto chini ya miaka mitano inapungua kwa kunyunyuzia
dawa ya ukoko kwa halmashauri tatu, matumizi ya chandarua, na utoaji wa
matibabu sahihi vituoni.
Mkutano huo wa tathmini ya
utekelezaji wa uboreshaji wa huduma za afya kwa watoto waliochini ya umri wa
miaka mitano umefanyika jana katika ukumbi wa mikutano na mafunzo wa anglikana
musoma.
0 comments:
Post a Comment