Klabu ya Manchester United imetweet: "Kufuatia uchunguzi wa kina, Robin
van Persie ameumia goti, ambalo litamuweka nje kwa kiasi cha wiki nne
hadi sita,".
Pamoja na kukosa mechi dhidi ya West Ham na Bayern
Munich katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Van Persie, ambaye amefunga mabao
17 msimu huu, atakosa pia mechi dhidi ya Manchester City Jumanne.
MECHI ATAKAZOKOSA RVP
Machi 23: West Ham (A)
Machi 25: Man City (H)
Machi 29: Aston Villa (H)
Aprili 1: Bayern Munich (H)
Aprili 5: Newcastle (A)
Aprili 9: Bayern Munich (A)
Aprili 20: Everton (A)
Aprili 26: Norwich (H)
(H ni mechi za nyumbani na A ni mechi za ugenini)
0 comments:
Post a Comment