NA AHMAD NANDONDE,
MUSOMA.
MWILI WA ALIYEKUWA
MKUU WA MKOA WARA BW. JOHN TUPPA UNATARAJIA KUAGWA KESHO NYUMBANI KWAKE KUANZIA
SAA MOJA KAMILI ASUBUH MPAKA SAA TATU NA DK 20 MUSOMA MKOANI MARA NA
BAADAE KUELEKA KANISA KUU LA ROMAN CATHOLIC PAROKIA YA MUSOMA KWAAJILI YA IBADA YA KUMUOMBEA MAREHEMU KUANZIA SAA TANO ASUBUHI HADI SA 9:00 JIONI.
HAYO YAMESEMWA LEO NA KATIBU TAWALA WA MKOA BW. BENEDICTOR OLE KUYAN ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI MCHAN WA LEO KATIKA UKUMBI MDOGO WA MIKUTANO.
OLE KUYAN AMESEMA KUWA MARA BAADA YA IBADA HIYO MWILI WA MAREHEMU UTASAFIRISHWA MPAKA KWENYE UWANJA WA NDEGE WA MWANZA AMBAPO UTAWASILI SAA KUMI NA NUSU ALASIRI KABLA YA KUSAFIRISHWA TENA HADI MJINI DODOMA AMBAPO UNATARAJI KUWASILI SAA KUMI NA MOJA JIONI NA KUHIFADHIWA KATIKA HOSPITAL YA MKOA.
KWA KUWA ENZI ZA UHAI WAKE MAREHEMU ALIWAHI KUFANYA KAZI MJINI DODOMA KAMA MKUU WA WILAYA WANANCHI MKOANI HUMO WATAPATA FURSA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU TAREHE 28 KUANZIA SAA TATU ASUBUHI HADI SAA SITA MCHANA.
BW. OLE KUYAN AMEONGEZA KUWA BAADA YA WAKAZI WA DODOMA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU SAA SITA MCHANA MWILI HUO UTASAFIRISHWA TENA HADI KIJIJINI KWAKE KILOSA AMBAPO UTAKABIDHIWA KWA FAMILIA YA MAREHEMU KWAAJILI YA MAOMBOLEZO SAA TISA ALASIRI.
MWILI WA MAREHEMU UTAFANYIWA IBADA IKIWA NI PAMOJA NA WANANCHI WA KILOSA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU KWA MARA MWISHO KABLA YA KUPELEKWA KATIKA ENEO LA MAZISHI KWAA JILI YA KUUHIFADHI KATIKA NYUMBA YA MILELE SAA KUIMI NA MOJA JIONI.
MAREHEMU TUPA AMEFARIKI DUNIA JANA WILAYANI TARIME ALIPOKUWA KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI NA AMEACHA MKE NA WATOTO WATANO.
MAREHEMU ALIZALIWA JAN 1 1950.
MWISHOOOO…
MWANDISHI WA HABARI WA CHANNEL TEN AUGASTINE MGENDI AKIMUULIZA KATIBU TAWALA SWALI HUKU WAANDISHI WENGINE WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI.
WAKATI WAKIPOKEA RATIBA YA KUUAGA MWILI WA MAREHEMU TOKA KWA KATIBU TAWALA.
@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@@
TAARIFA TOKA TAASISI
YA WAANDISHI WA HABARI MKOANI MARA YA MARA HOPE FOR LIFE (MHL)
TODAY AT 12:36 AM
BIGAMBO JEJE,MUSOMA
MARCH 26 2014,
TUPPA.
TAASISI YA WAANDISHI WA
HABARI MKOANI MARA YA MARA HOPE FOR LIFE (MHL) IMEMTUMIA SALAMU ZA RAMBIRAMBI
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHE:DK JAKAYA KIKWETE KUFUATIA KIFO CHA
MKUU WA MKOA WA MARA JOHN GABRIEL TUPPA ALIYEFARIKI DUNIA KWA GHAFLA AKIWA
KATIKA KAZI ZA KUWATUMIKIA WANANCHI.
MKURUGENZI MKUU WA
TAASISI HIYO YA WANAHABARI WA MKOA WA MARA BW. FAZEL JANJA AMEMUELEZEA MAREHEMU
TUPPA KWAMBA WATANZANIA DAIMA WATAMKUMBUKA KWA MAMBO MENGI KATIKA KUWATUMIKIA
WATANZANIA KATIKA NYADHIFA MBALIMBALI ALIZOZITUMIKIA KATIKA UADILIFU NA UAMINIFU
MKUBWA.
BW. JANJA AMESEMA WAKATI
WA UHAI WAKE HUSUSANI TANGU ALIPOTEULIWA NA RAIS KIKWETE KUTUMIKIA WADHIFA WA
UKUU WA MKOA WA MARA MWAKA 2011, MAREHEMU ALIJITOLEA KWA HALI YAKE YOTE
KUHAKIKISHA ANAWAHUDUMIA WANANCHI KATIKA KUWALETEA MAENDELEO KATIKA NYANJA
KADHAA ZA ELIMU,MIUNDO MBINU,AFYA,MAJI NA KILIMO HUKU AKIMSIKILIZA KILA
MWANANCHI NA KUTATUA KERO ZAO KWA KUTENDA HAKI BILA AINA YOYOTE ILE YA AMA
UBAGUZI AU UPENDELEO.
AMETANABAISHA KWAMBA
MAREHEMU TUPPA AMBAYE KIFO CHAKE NI PIGO KUBWA NA KIMEACHA PENGO LISILOWEZA
KUZIBIKA KWA URAHISI, ENZI YA UHAI WAKE ALISHIRIKIANA NA VYAMA VYOTE
VYA SIASA KATIKA SHUGHULI ZA KIMAENDELEO HUKU AKIWAITA NA KUKAA NAO ILI
KUJADILI NAMNA YA KUWEZA KUUENDELEZA MKOA KWA KUSHIRIKIANA KWA PAMOJA BILA
KUWEKA TOFAUTI ZA VYAMA VYAO.
SALAMU HIZO ZA
RAMBIRAMBI KWENDA KWA MHE:RAIS KIKWETE ZIMEONGEZA KUWA WAANDISHI WA HABARI
MKOANI MARA WALIPATA USHIRIKIANO MKUWA NA WA KARIBU SANA TOKA KWA MAREHEMU
TUPPA AMBAYE DAIMA ALIWAPENDA WANAHABARI NA KUWAPA KILA AINA YA USHIRIKIANO
WALIOUTAKA TOKA OFISINI KWAKE NA KWAMBA KIFO CHAKE KIMEACHA PIA MAJONZI,SIMANZI
NA HUZUNI ISIYO NA KIFANI KWA WANAHABARI WOTE.
MKURUGENZI HUYO MKUU WA
TAASISI HIYO YA MHL BW. JANJA AMEWATAKA VIONGOZI KUIGA MFANO WA MAREHEMU TUPPA
KATIKA KUWATUMIKIA WANANCHI KWA KILA HALI NA KWA MOYO WA KUJITOLEA NA
KUSISITIZA KUWA HATUA YA KUKUTWA NA UMAUTI AKIWA KAZINI NI USHUJAA,USHUPAVU NA
UJASIRI MKUBWA AMBAO DAIMA JINA LAKE LITAANDIKWA KATIKA HISTORIA YA MASHUJAA WA
HAPA NCHINI.
AIDHA AMEIOMBA FAMILIA
YA MAREHEMU ALIYEFARIKI KUTOKANA NA SHINIKIZO LA DAMU AKIWA KIKAZI WILAYANI
TARIME, KUWA NA UVUMILIVU,USTAHIMILIVU NA SUBIRA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU
WANACHOPITIA NA KUJIPA MOYO INGAWA KILA MMOJA ANATAMBUA KWAMBA MAREHEMU
AMETANGULIA MBELE ZA HAKI HUKU FAMILIA HIYO IKIWA BADO INAMUHITAJI.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment