Na Derick Milton Simiyu,
TATIZO la kukati katika kwa umeme linalowakabili wakazi wa wilaya
ya Maswa mkoa wa Simiyu juzi lilizua balaa katika hospitali ya wilaya hiyo
baada ya muunguzi katika wodi ya akinamama wajawazito kuzalisha akinamama
wawili gizani huku akitumia tochi ya simu aina ya Nokia kutokanana kukosekana
kwa nishati ya umeme.
Tukio hilo lililotokea mwishoni mwa juma majira ya saa 1:00 usiku muda mfupi baada ya umeme kukatika na hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa akina mama hao ambao walikuwa wakipiga kelele za kuomb
Watu walioshuhudia tukio hilo walisema kuwa licha ya hospitali kuwa na jenereta ambayo hutumika mara baada ya umeme kukatika lakini siku hiyo haikuweza kuwasha kutokana na mhusika kutokuwepo eneo hilo.
Bi Ziada Khamis ambaye alishuhudia tukio hilo alisema kuwa alifika hospitalini hapo kwa ajili ya kupima BP ambapo mashine iko katika wodi ya akina mama wajawazito lakini ghafla umeme ulikatika lakini muuguzi aliyemkuta alikuwa katika chumbacha akinamama kujifungulia.
Alisema kuwa wakati akiwa akisubiri kupata huduma hiyo mara ghafla alisikia sauti za akina mama waliokuwemo ndani ya chumba hicho wakiomba msaada ndipo alipomuuliza muuguzi ambaye alimwomba aje amshikie simu yenye tochi ili aweze kuwasaidia akina mama kujifungua kutokana na kukosekana kwa umeme.
“mie ndiye niliyeshuhudia tukio la huyo muuguzi kuzalisha gizani siku ya jumamosi tarehe 25.01.2014 akitumia mwanga hafifu wa tochi ya simu aina ya Nokia na alikuwa pekee yake kwani mwenzake alikwenda kuwaomba walinzi wawashe jenereta lakini wakasema mhusika hayupo hivyo ikabidi nimsaidie kushika tochi ili aweze kuzalisha”alisema Ziada Khamis.
Bi Ziada ambaye pia ni Diwani wa viti maalum(Chadema)katika halmashauri ya wilaya hiyo alisema kuwa kitendo hicho kinawafanya wauguzi katika hospitali hiyo kufanya kazi katika mazingira magumu huku akitupia lawama uongozi wa hospitali ya wilaya ya Maswa.
‘hapa ni lazima Mganga Mkuu awe makini sana vinginevyo hali hii ikiendelea inaweza kusababisha vifo visivyotarajiwa kwa akina mama wajawazito na watoto watakaojifungua nalikitokea jambo hilo wanaolaumiwa ni wauuguzi walioko katika wodi lakini na wenyewe wanafanya kazi kazi katika mazingira magumu”alisema kwa masikitiko.
Baadhi ya wauguzi ambao waliongea na Mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutotaka majina yao yaandikwe gazetini walilalamikia uongozi wa hospitali hiyo kwani umeme unapokatika inachukua muda mrefu kuwashwa kwa jenereta hivyo kuwafanya wafanye kazi katika mazingira magumu.
“mie lawama nazitupa kwa uongozi wa hospitali hili suala tumelilalamikia kwa muda mrefu sana na ndiyo maana siye tulio wengi tunatumia simu zenye tochi maana ukiwa zamu ya usiku umeme ukikatika ndiyo zinatusaidia kuwahudumia akinamama wenzetu hasa wanaojifungua kwa nyakati hizo”alisema mmoja wao.
Waliendelea kueleza kuwa kuzalisha kwa kutumia tochi ya simu ni jambo la hatari kwani kunaweza kumsababishia madhara mama mjamzito iwapo simu hiyo ikamdondokea lakini hawawezi kuacha kuwasaidia kwa kukosa umeme huku wakisisitiza kuwa Mungu ndiye anayewasaidia.
Akizungumzia malalamiko hayo Mganga Mkuu wa wilaya ya Maswa,Dk Jonathan Budemu amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kueleza kuwa ameanza kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuweka bajeti ya kununua mashine ya kufua umeme ambayo itakuwa inajiunganisha pindi umeme unapokatika.
‘tatizo hili lipo na hasa umeme unapokatikakatika mara kwa mara hivyo tumekaa tumeona ili kulimaliza tatizo hili ni kununu jenereta ambavyo itakuwa ni atomatic kwani umeme wa Tanesco ukikatika inajiwasha mara moja na hata kama mgonjwa anapasuliwa kazi inaendelea kama kawaida”alisema.
Mwisho.....



0 comments:
Post a Comment