Home »
MICHEZO
» Yanga yafanya kikao kizito kuiua St. Louis
 |
Saa chache kabla ya pambano lao dhidi ya St. Louis, benchi la ufundi na wachezaji wa Yanga wamekaa kikao cha takribani saa moja na nusu kuweka mikakati ya mwisho ya kuwamaliza wapinzani wao. Kikao hicho kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Reef Holiday ambako timu hiyo imefikia tangu ilipofika Shelisheli. Kikao hicho cha kupeana mikakati na mbinu za kiufundi, kiliongozwa na Kocha Mkuu, George Lwandamina na wasaidizi wake Nsajigwa Shadrack na Noel Mwandila. Hali ya usiri ilitawala katika kikao hicho kwani zaidi ya wahusika, hakuna mtu mwingine aliyeruhusiwa kuhudhuria.
|
0 comments:
Post a Comment