`

Home » » MANISPAA YA MUSOMA YAGAWA MADAWATI

MANISPAA YA MUSOMA YAGAWA MADAWATI

Musoma.
Kufuatia kuwapo kwa changamoto kubwa ya uhaba wa madawati katika shule nyingi zilizopo katika manispaa ya musoma jumla ya madawati 357 yametolewa jana katika shule za msingi zipatazo 20 katika manispaa hii.

Akizungumza wakati wa kukabidhi madawati hayo meya wa manispaa ya musoma bw. Alex Kisurura amesema kuwa mbali na kuwepo kwa shughuli nyingi za maendeleo lakini kamati ya mfuko wa jimbo imeonelea kuanzia katika sekta ya elimu kwa kugawa madawati katika shule.

Mbali na madawati hayo 357 kutolewa kwa shule za msingi lakini pia jumla hya madawati 80 yametolewakwa shule za sekondari zipatazo kumi kwaajili ya kupunguza uhaba wa madawati katika shule zilizopo ndani ya manispaa ya musoma.

Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Iringo 'A' Bi. Consolata Naftal ameushukuru mfuko wa jimbo kwa msaada huo kwani wapo walimu ambao hawakupata msaada huo mbali na msaada huo kuwa ni mdogo lakini utaweza tatizo hilo ingawa si kwa kuondoa kabisa tatizo hilo kwani pamoja na msaada huo lakini bado shule yake inahitaji madawati 101.

Zaidi ya shilingi mil. 44 zimetumika katika utengezaji wa madawati hayo kwa shule za msingi na zaidi ya shilingi mil. 24 kwa madawati ya shule za sekondari.

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK