MUSOMA.
WITO UMETOLEWA KWA WANANCHI WENYE MAPENZI MEMA KWA TAIFA HILI MKOANI MARA KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA SIRI KWA JESHI LA POLISI ILI KUHAKIKISHA MATUKIO YA UHALIFU YANAKOMESHWA KABISA MKOANI HAPA.
HAYO YAMESEMWA JANA NA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI BW. ISSAYA MNGULU ALIPOKUWA AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KATIKA OFISI YA KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA
MNGULU AMESEMA KUTOKANA NA MATUKIO HAYO NI WAZI KUWA WANANCHI WA TARAFA YA NYANJA NA MAENEO MENGINE NCHINI WANATAKIWA KUJIJENGEA TABIA YA KUIMARISHA ULINZI NA HATA KUONGOZANA KATIKA SHUGHULI ZA KILIMO ILI KUONDOA MWANYA KWA WAHALIFU KUFANYA MATUKIO HAYO YA MAUAJI HALI ITAKAYOPELEKEA WANANCHI HUSUSAN WANAWAKE KUFANYA KAZI ZAO BILA HOFU YA KUUAWA.
UJIO WA MNGULU MKOANI HAPA UNA LENGO LA KULIONGEZEA NGUVU JESHI LA POLISI KWA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA KUFUATIA MATUKIO YA MAUAJI YA WANAWAKE WANANE WALIOFARIKI KWA KIPINDI CHA MWEZI JAN HADI SASA ILI SHERIA IWEZE KUCHUKUA MKONDO WAKE.
MNGULU AMESEMA KATIKA MATUKIO HAYA IMEBAINIKA KUWA YAPO MAMBO MENGI AMBAYO YANAFANANA IKIWEMO VIFO HIVYO KUWALENGA ZAIDI WANAWAKE, KUUAWA WAKIWA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA KILIMO HUSUSAN NYAKATI ZA MCHANA, KUUAWA KWA KUNYONGWA AIDHA KWA KAMBA AU KANGA NA HATA KUPIGWA NA VITU VYENYE NCHA KALI AU BUTU KICHWANI.
AMESEMA MBALI NA HAYO LAKINI PIA BAADA YA WANAWAKE HAO KUUAWA HUFUKIWA KWENYE MASHIMO MADOGO AU KUTUPWA VICHAKANI HUKU WAKIACHWA HAWANA NGUO.
MWISHO......
DCI ISSAYA MNGULU
0 comments:
Post a Comment