HIJABU
YA MWANAMKE WA KIISLAM
KATIKA
QUR-AN NA SUNNA
Ni kweli na ni hakika kwamba inasikitisha sana kwa wanawake mbali mbali wa Kiislam kwa namna ya mavazi wanayovaa kila siku zinavyokwenda, siku hizi wanawake wengi wamekuwa wakivaa mavazi yasiyo na stara, wanavaa mavazi ya kikafiri, ambapo ukiwaangalia utaona kuwa hakuna tofauti baina yao na Mayahudi au hata Wakristo, na hali hii imekuwa ni hatari kubwa sana katika maisha ya Uislam, na kupelekea au kusababisha kushuka kwa hasira ya Mwenyezi Mungu na yakateremka maangamizo na kuangamia wema na wabaya.
Na lengo ni wale mawalii amri wa hao wanawake wanawaachia wake zao na mabinti zao na dadfa zao kuvaa nguo za kikafiri na kutoka nje ya nyumba zao bila ya kuvaa baibui na hijaab. Na yakizodi mambo haya ni sababu ya kushuka maangamizo kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote wabaya na wema.
Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Surat Al-Anfaal aya ya 25 amesema:-
“NA IOGOPENI ADHABU YA MWENYEZI MUNGU HAPA DUNIANI AMBAYO HAITAWASIBU PWKW YAO WALE WALIODHULUMU NAFSI ZAO MIONGONI MWENU BALI ITAWASIBU HATA WALIONYAMAZA WASIYAKATAZE MAOVU. NA WENGINEO PIA. NA JUENI YA KWAMBA MWENYEZI MUNGU NI MKALI WA KUADHIBU.”
Kutokana na ukali wa aya hiyo ya Mwenyezi Mungu enyi Mawalii amri wakatazeni wake zenu mabinti zenu na dada zenu, na waamrisheni waisitiri miili yao, na iogopeni adhabu ya Mwenyezi Mungu, la si hivyo mtasababisha kuwashukia hasira ya Mwenyezi Mungu kwa wote.
Uislam ni Dini iliyoleta sheria na adabu za Kiislam, na baadhi yake ni sheria ya vazi la Kiislam kwa wanawake wa Kiislam.
Wanawake wa kiislam wamekuwa na tabia mbaya iliyo kinyume na maamrisho ya dini yao kwa kwenda makazini kukaa mabarazani au hata kupita katika masoko wakiwa uchi, wanaonesha miili yao ovyo kwa wanaume wanaoweza kuwaoa (Ajnabi) bila hata kuwa na hofu juu ya Mola wao au hata kuona haya ama aibu ya aina yeyete ile. Na tabia hii ni katika mambo mabaya sana na ni hatari kubwa sana katika jamii ya Kiislam kwa haya maasi makubwa kabisa yanayofanywa na wanawake ikiwa ni dada zetu mama zetu wake zetu au hata mabinti zetu na hata wa wenzetu.
Hijaab ya mwanamke wa Kiislam imekuja kwa malengo maalum kama sheria ya kustiri miili ya wanawake, kwa kuamrishwa wanawake wa Kiislam kuisitiri miili yao kwani kufanya hivyo ni salama kwao na ni kuepukana na Shetani kwa kufanya mambo machafu na mengine yaliyokuwa mabaya na yenye kuvutia matamanio mabaya.
Sharia ni lazima kwa kila walii, ambao ni wazazi, au waume au kaka au ndugu, na wanatakiwa wasinyamaze na kuwaregezea watu wao wa kike kutoka katika misingi ya sheria na adabu ya Kiislam.
Tabia hii ya kuwaachia wanawake inawapasa (wanaume) au hata wanawake kuikataza jamii nzima ya wanawake wa Kiislam na wasiachiwe kabisa kuvaa mavazi ya kikafiri na kutoka nayo nje bila ya kusitiri miili yao.
Faradhi hii ni ya kila Muislam ya kuamrisha mema na kukataza mabaya, kwani kunyamaza kimya bila ya kukataza mabaya ni sababu kubwa ya kutyokea maafa mbali mbali katika jamii ya Waislam na hatimae kufikwa na maangamizo.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:-
“HAKIKA WATU WANAPOONA MABAYA YANAFANYIKA KISHA WASIYABADILI KWA KUYAKATAZA, WAKANYAMAZA NA KUPUUZA BASI IMEKARIBIA KUWASHUKIA ADHABU YA MWENYEZI MUNGU”
Na katika Qur-an Mwenyezi Mungu Mtukufu sehemu nyingi amesimulia habari za maangamizo waliyoangamizwa watu wa Israil kutokana na kutokataza mabaya, walikuwa wanaona mabaya yanafanyika laini walibyamaza kimya bila ya kukatazana, na hapo ndipo ilipowashukia laana na adhabu ya Mwenyezi Mungu juu yao kutokana na kunyamaza kimya kwao.
Katika Surat Al-Maaida aya ya 78/79 Mwenyezi Mungu amesema:-
“WALILAANIWA WALE WALIOKUFURU MIONGONI MWA WANA WA ISRAIL KWA ULIMI WA NABII DAUD NA NABII ISSA IBN MARYAM. HAYO NI KWA SABABU WALIASI NA WAKIRUKA MIPAKA YA MWENYEZI MUNGU. HAWAKUWA WENYE KUKATAZANA MAMBO MABAYA WALIYOKUWA WAKIYAFANYA, MAOVU YALIOJE YA MAMBO HAYO MABAYA WALIYOKUWA WAKIYAFANYA.”
Hiyo ndiyo hatari ya kuyaona mabaya yanafanywa kasha watu wakanyamaza kimya bila hata kuyakataza.
Sasa hao mawalii (wazee ikiwa ni wanaume au hata wanawake) wa kina dada, wake au mabinti ndio waliolazimika kuyasimamia na kuwakataza wanawake kuvaa mavazi ya kikafiri sio kuregeza na kunyamaza kimya.
Lakini utakuta hao mawalii wenyewe wamenyamaza, na kunyamaza kwao ina maanishwa kuwa wako radhi kuwaachia watoto wao, wake zao, dada zao au hata mama zao kuonesha miili yao kwa watu ajnabi. Na hii ndio sababu ya kushuka hasira na adhabu za Mwenyezi Mungu wakaangamia wema na wabaya kutokana kunyamaza kwa kutoyakataza mabaya.
Basi hapo laana ya Mwenyezi Mungu humpata kila mtu. Na ni sababu za maangamizo zinakuwa namana hiyo za kutokataza mabaya na kunyamaza kimya.
Na hao mawalii wananyamaza na kuwaachia wake zao na dada zao na watoto wao kuvaa nguo za kubana na kutoka nje bila ya kuvaa hata baibui, wanaonesha miili yao ovyo huko nje. Kila mtru ajnabi huko nje anausoma mwili wa mwanamke ulivyo, na hali huyo mwanamke ni Muislam.
Tujiulize je huyo tutamwita kuwa ni mwanamke wa Kiislam? Kichwa chake kiwazi na ikiwa kajitanda basi huo mtandio si wa sitara, bali mtandio wa pambo tu, kichwa chote kinaonekana.
Au atafunika kichwa vizuri kwa huo mtandio au ushungi lakini, lakini kava nguo za kubana, mwili wake wote unaonekana, unamuona viumgo vyote vya mwili wake, jee! Huyo tuamwita mwanamke wa Kiislam?
Mwanamke wa namna hiyo yeye na kafiri ni sawa kabisa, hana Uislam wowote, na hali ya kuwa Uislam umeleta sheria ya vazi la wanawake wastiri miili yao.
Mwenyezi Mungu Mtukufu alipokuwa akiwahutubia wake wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambapo hotuba inayowahusu wake wa mtume ni kwa ajili ya Waislam wote.
Amesema katika Surat Al Ahzab aya ya 33:-
“NA KAENI MAJUMBANI MWENU WALA MSIONESHE MAPAMBO YA MIILI YENU KAMA WALIVYOKUWA WAKIONESHA MAPAMBO YAO WANAWAKE WA ZAMA ZA UJAHILIYA.”
Wafasiri wa aya hii wamesema maana ya “TABARRUJIL-JAAHILIYYAH” Ya kuwa ni kuonesha mwanamke namna ya pambo la mwili wake ulivyo ili avutike mwanamme aingiwe na matamanio mabaya ya zanaa.
Katika zama za ujahiliya mwanamke alikuwa anajitahidi kuupamba mwili wake na kuvaa nguo za kubana na nyepesi ili mwili wake uonekane vizuri na wanaume, basi mwanamme yeyote tule akimuona tu mwanamke alievaa nguo za kubana namna hiyo akauona mwili wa mwanamke huyo, hupiga katika moyo wake tamanio baya unamsadikisha na kuingia katika maovu ya kuzini. Hivi ndivyo walivyotafsiri wataalam juu ya maana ya “TABARRUJIL-JAAHILIYYAH” Ni kwamba kuonesha pamno la mwili wake mwanamke ili avutike mwanamme kwa tamanio la zinaa.
Vile vile maana ya “TABARRUJIL-JAAHILIYYAH” imetafsiriwa kuwa ni kuonesha mwili wake mwanamke na kutembe utembezji wa kudeka na kulainika mwili wake na kuilegeza miguu yake katika mwendo wake wa kuilegeza shingo yake ili kichwa chake kilegee kwa kunyongeka na kulainika kama ilivyolainika nundu ya ngamia, maana wale ngami walionona wakitembea nundu zao hulainika na hunama mara kulia na mara kushoto.
Basi wanawake waliotajwa kuhusu “TABARRUJIL-JAAHILIYYAH” ndio vichwa vyao sawa na hizo nundu za ngamia, na kuvaa nguo ambazo si za stara.
Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:-
“WANAWAKE WAMEVAA MAVAZI YA UCHI (YAANI NGUO SI ZA STARA) WAMEELEMEA KUINAMA (KUPENDA MAVAZI YASIYOKUWA YA STARA), VICHWA VYAO KAMA NUNDU ZA NGAMIA VIMEINAMA HAWATAINGIA PEPONI WALA HAWATAPATA (HATA) HARUFU YAKE (PEPO).”
Ndio nguo wanazovaa wanawake siku hizi za kukaa uchi tu, si nguo za stara, bali nguo za mapambo ya kuonesha miili yao, ambazo alizozitaja Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Na Mwenyezi Mungu kabainisha namna ya nguo za Kiislam na sheria kwa mwanamke wa Kiislam amelazimisghwa avae kwa ajili ya kusitiri mwili wake. Mwenyezi Mungu anamwambia Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) awaambie wanawake wa Kiislam katika Surat Nuur aya ya 31:-
“NA (EWE NABII MUHAMMAD) WAAMBIE WAISLAM WANAWAKE WAINAMISHE MACHO YAO, NA WAZILINDE TUPU ZAO WALA WASIDHIHIRISHE VIUNGO VYAO VYA MWILI KWA WATU ISIPOKUWA VINAVYODHIHIRIKA KAMA USO NA VIGANJA VYA MIKONO, NA WAANGUSHE SHUNGI ZAO AU MITANDIO MPAKA VIFUANI MWAO, NA WASIONESHE MAPAMBO YAO ILA KWA WAUME Z\AO, AU BABA ZAO, AU BABA ZA WAUME ZAO, AU WATOTO WAO, AU WATOTO WA WAUME ZAO, AU KAKA ZAO, AU WATOTO WA KAKA ZAO, AU WATOTO WA DADA ZAO, AU WANAWAKE WENZAO, AU WALE ILIYOMILIKI MIKONO YAO YA KUUME, (YAANI WATUMWA WAO) AU WAFUASI WA WANAUME WASIOKUWA NA MATAMANIO YA WANAWAKE, AU WATOTO AMBAO HAWAJAJUA MAMBO YANAYOHUSU UKE, WALA WASIPIGE MIGUU YAO ILI YAJULIKANE WANAYOYAFICHA KATIKA MAPAMBO YAO. NA TUBIENI NYOTE KWA MWENYEZI MUNGU, ENYI WAISLAM ILI MPATE KUFUZU.”
Sasa hiyo ni amri ya Mwenyezi Mungu anakataza wanawake kuonesha miili yao, waisitiri kweli kweli, sio kuiweka wazi miili yao ikawa inaonekana na watu ovyo. Jee huo ndio Uislam? Ukweli ni kwamba huo si Uislam kabisa huko ni kwenda kinyume na sheria za Mwenyezi Mungu.
Wanaamrishwa wanawake waisitiri miili yao, pamoja na kuinamisha macho yao wanapopita mbele za watu, wasipepese macho kutazama watu. Kama walivyoamrishwa wanawake wainamishe macho yao basi pia hata wanaume wameamrishwa wainamishe macho yao wanapopita mbele ya wanawake, wasipepese macho yao kutazama wanawake, na amri hiyo pia ni katika Surat Nuur katika aya ya 30:-
“SEMA (EWE NABII MUHAMMAD) UWAAMBIE WAISLAM WANAUME WAINAMISHE MACHO YAO (WASITAZAME WANAWAKE AU YALIYOKATAZWA), NA WAZILINDE TUPU ZAO, (ILI WASIINGIWE NA MATAMANIO MABAYA), KUFANYA HIVYO NI TAKASO KWAO (WANATAKASIKA NA KUEPUKANA NA MARADHI YA MACHAFU YA ZINAA.)”
Kwa sababu mwanamme akimtazama mwanamke siejietiri mwili wake, viungo vya mwili vyote vinaonekana, basi mwanamme huingiwa na tamanio baya la zinaa, na hiyo ndio hatari yenyewe. Na wanawake wasiositiri miili yao, basi wanawasababishiwa wanaume kupata madhambi.
Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):-
“MWENYE KUTAZAMA UZURI WA MWANAMKE AJNABI KWA MATAMANIO (MACHAFU YA ZINAA, BASI) HUMWAGIWA MACHONI MWAKE RISASI ILIYOYEYUSHWA KWA (MOTO) SIKU YA KIAMA.”
Kwa hivyo sasa hatari ya manaume inawata kwa sababu ya wanawake wasiojistiri miili yao. Hii ndio sababu Mwenyezi Mungu anaamrisha kwa wanaume na wanawake kuinamisha macho yao ili wasalimike na mambo yanayovutia machafu ya zinaa.
Lakini mwanamke ikiwa hakuustiri kwa kuuficha mwili wake kwa nguo za stara kama ilivyoamrishwa na sheria ya Uislam, jee mwanamme ataweza kuinamisha macho yake? Kwa kuwa mwanamke kava nguo za kubana, na mwili wake wote unaonekana ulivyo, viungo vyote unaweza kuvihesabu na kuviona vilivyo, ina maanisha umbo lake lote unaliona alivyoumbwa, hakuna tofauti yoyote na aliyekaa uchi. Jee! Huyo mwanamke kaustiri mwili wake? Huyo si yuko uchi tu.
Sasa mwanamme akiona mwanamke alievaa vazi hilo ataweza kuinamisha macho yake? Kwa sababu kuna wanaume wengine wana maradhi ya tabia chafu, na anataka tu na kupenda atazame mambo kama hayo. Baada ya kuinamisha macho yake, basi ndio atazidi kuinua macho yake na kuyafungua zaidi ili aone kiroja cha mwili wa huyo mwanamke.
Na hapo sasa ndio Shetani anaingia baina yao, yule mwanamme moyo wake unamuanguka, na utupu wake unamsadikisha kwa matamanio machafu ya zinaa. Na hapo sasa yule mwanamke atakuwa kishazini na yule mwanamme aliyouona mwili wa yule mwanamke, ijapokuwa hawakulala kitanda kimoja.
Na yule mwanamke anakuwa katika hukumu ya kuzini, na anapata dhambi za kuzini, na kuwa na hukumu ya janaba katika mwili wake. Na lazima kwanza aende akakoge ukogakji wa janaba, na haimjuzii kusali wala kufanya ibada yoyote, kwa ajili ya kuweka mwili wake wazi ukaonekana na watu ajnabi, kwani macho nayo yanazini.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:-
“KILA JICHO LIMEZINI”
Ina maanisha kuwa kila jicho la mtu aliyemtazama yule mwanamke basi kazini na yule mwanamke aliyekuwa hajajistiri mwili wake kwa kuuacha mwili wake waziukaonekana na wanaume ajnabi.
Kwa hivyo mwanamke wa aina hiyo asiejistiri mwili wake, basi tangu ametoka nyumba kwake katika safari zake mpaka mpaka anarudi nyumbani kwake au kwao, jee jiulize ni macho mangapi ya watu yaliyomtazama huyo mwanamke? Ikiwa ni watu kumi au elfu, basi wote hao amezini nao, na anapata madhambi ya kuzini na watu wote hao waliouona mwili wake.
Na hiyo ndiyo “TABARRUJIL-JAAHILIYYAH” iliyotajwa katika Surat Al-Ahzab tuliyoifasiri hapo nyuma. Na hali Mwenyezi Mungu kawakataza wanawake wa Kiislam waache kabisa wasifanye hayo mambo ya kijahiliya. Na leo wanawake wa Kiislam wanaurejesha wenyewe ujahiliya na wanakanusha amtri ya Mwenyezi Mungu aliyoamrisha waistiri miili yao wanawake wa Kiislam.
Jee hiyo si hatari kubwa kabisa? Basi mwanamke wa namna hiyo kila siku anapata mambo haya yafuatayo:-
(a). Anapata laana ya Mwenyezi Mungu na hasira yake, na analaaniwa na kila anaelaani.
(b). Anapata dhambi za kuzini.
(c). Daima anakuwa katika hukumu ya mwili mchafu wa janaba.
(d). Sala yake wala ibada yake yoyote haikubaliwi, wala haipandishwi amali yake mbinguni hata shibiri moja.
(d). Hukumu yake anakuwa katika idadio ya miongoni mwa mkafiri, na wala si Muislam tena unamtoka Uislam kabisa.
Na mwanamke wa aina hiyo asiekuwa na haya wala kumuogopa Mola wake, basi huyo ni kafiri tu. Maana tabia ya dini ya Kiislam basi mtu ni kuwa na haya.
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:-
“NA KILA DINI INA TABIA, NA TABIA YA DINI YA UISLAM (MTU KUWA NA) HAYA (AIBU).”
Na mwanamke aneuonesha mwili wake wote mabarabarani na katika afisi za kazi na hadi katika masoko bila ya kuona haya wala kumuogopa Mola wake. Hajali kabisa hayo, anapita barabarani kichwa wazi, au kafunika kichwa lakini mwili wake wote uko wazi na kava nguo za kubana, au nguo fupi. Hiyo ndiyo “TABARRUJIL-JAAHILIYYAH” . Yeye na kafiri hawana tofauti.
Au tukitazama katika Surat Al-Ahzab tunaona Mwenyezi Mungu anaamrishwa zaidi wanawake waisitiri miili yao, maana kustiri miili yao basi ni salama yao wenyewe, na wanaepukana na na udhia kutokana na watu wenye tabia mbaya. Mwenyezi Mungu katika Surat Al-Ahzab aya ya 59 amesema:-
“EWE NABII (MUHAMMAD)! WAAMBIE WAKE ZAKO, NA MABINTI ZAKO, NA WANAWAKE WA WAISLAM (YA KWAMBA) WAZITEREMSHE NGUO ZAO (KWA KUSTIRI MIILI YAO,) KUIFANYA HIVYO NI KUWAPELEKA UPESI WAJULIKANE (YA KWAMBA WAO NI WANAWAKE WENYE HESHIMA) ILI WASIUDHIWE NA WATU (WENBYE TABIA MBAYA), NA MWEYEZI MUNGU NI MWINGI WA KUSAMEHE NA MWINGI WA KUREHEMU.”
Sasa hapa Mwenyezi Mungu anaamrisha wanawake wa Kiislam wazidi kuisitiri miili yao. Maana miili ya wanawake kuiweka wazi ikaonekana na wanaume ajnabi ndio sababu kubwa kwa Shetani kuvutia mambo machafu ya zinaa. Na wanawake ndio fitna (ina maana kuwa) mtihani mkubwa sana kwa wanaume kufanya mambo machafu ya zinaa.
Mwenyezi Mungu katika Surat Al-Imraan aya ya 14 amesema:-
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
HIJABU VAZI LIMFAALO MWANAMKE WA KIISLAMU.
BINTI WA KIISLAMU AKIWA KATIKA VAZI LA HIJABU.
TAZAMA AKINA DADA WAKIWA WAMEVALIA HIJABU KATIKA MICHEZONI.
AKINA MAMA WA KIISLAMU NDANI YA MAVAZI YAO MARIDADI.
0 comments:
Post a Comment