`

Home » » IMANI ZA KISHIRIKINA ZATAWALA PAMBANO LA WATANI WA JADI.

IMANI ZA KISHIRIKINA ZATAWALA PAMBANO LA WATANI WA JADI.


Katika hali ya kushnagaza leo katika mchezo wa watatani wa jadi  Simba na Yanga kumetokea kituko cha aina yake pale Didie Kavumbagu wa Yanga alipokosa Goli langoni na hivyo kuamua kulichukua taulo la mlinda mlango wa simba Ivo Mapunda na  Kukimbia nalo na kulitupa kwa watazamaji.

Tangu mlinda mlango huyo wa simba toka aliporejea nchini mara kwa mara amekuwa akionekana na taulo ambalo wengi wetu huwa tunaona kama ni kwaajili ya kufutia jasho awapo katika milingoti mitatu lakini kwa wapinzani mara nyingi wamekuwa na imani kuwa ni sehemu ya kuzuia magoli yasiingie langoni mwake.

Baada ya tukio hilo npambano ulilazimika kusimamishwa kwa muda baada ya wachezaji hao kuanza kukamatana jezi huku ivo akionekana kulihitaji taulo lake na Didier akidai kuwa linazuia magoli kuingia langoni mwa wekundu hao ingawa mwishoni Taulo hilo la aajabu lilirudishwa kwa Ivo Mapunda na Mchezo Kuendelea.

mpaka mwisho wa mchezo huo hakuweza kupatikana mbabe na matokeo yakawa ni 1-1 huku goli la Simba likiwekwa kimiani na Aroun Chanongo huku la yanga likiwekwa kimiani na Simon Msuva.


0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK