`

Home » » MTOTO WA MATUMLA AAHIDI KULIPA KISASI CHA BABAAKE MDOGO ASEMA ATAMGARAGAZA FRANCISE MIYEYUSHO HAPO APRIL 26.

MTOTO WA MATUMLA AAHIDI KULIPA KISASI CHA BABAAKE MDOGO ASEMA ATAMGARAGAZA FRANCISE MIYEYUSHO HAPO APRIL 26.


MABONDIA Fransic Miyeyusho 'Chichi Mawe' na Mohamed Matumla 'Snake JR' wanatarajia kuzinyuka april 26 katika ukumbi wa PTA Sabasaba. 

Mpambano uho utakaopigwa april 26 katika ukumbi wa pta sabasaba kutakuwa na mapambano mengine makali ya utangulizi ambapo mwana dada Lulu Kayage atamvaana na Halima Ramadhani siku hiyo kwa ajili ya kuhamasisha wanawake wenzao wajitokeze katika mchezo wa masumbwi.

Baada ya kusaini mkataba huo bondia Miyeyusho alijitapa kuendeleza ubabe katika familia hiyo ambapo alisema atamchakaza kama alivyo mchakaza baba yake mdogo Mbwana Matumla ambaye amecheza nae mara tatu na kupigwa mara mbili ambapo mpambano wa mwisho ulikuwa na shamu shamu nyingi kila upande miyeyeyusho alibuka mshindi kwa pointi.

Nae Matumla alijibu mapigo kwa kusema Miyeyusho anamuheshimu kwa kuwa yeye ni mkubwa kiumri hata hivyo atampa kichapo kikali kama alivyompatia mdogo wake Doi Miyeyusho ambaye mara ya kwaza alipigwa kwa K,O raundi ya pili DDC Keko na mara ya pili pia K,O ya raundi ya pili katika ukumbi uho uho uho wa PTA Sabasaba.
 
Amesema mbali na hayo lakini nia yake kubwa ni kutaka kulipiza kisasi cha babaake mdogo Mbwana Matumla ambaye mwaka juzi alipokea kichapo toka kwa bondia francise miyeyusho na hivyo kuahidi kutoshusha rekodi yake. 
 
Ameongeza kuwa yeye anayo kila sababau kuhakikisha anshinda katika mpambano huo nakumtahadharisha miyeyusho kuwa kama anataka kujua yeye ni mkali mkali zaidi ya familia yake yote amulize Prince Nassibu Ramadhani ambaye mwezi miezi miwili iliyopita alipatai kipigo cha paka mwizi na Moh'd Matumla na hivyo kujinyakulia pikipiki mpya.
 
Mpambano huo umedhaminiwa na Bw. Ally Mwazoa.
 
Mwisho.....

                                              MOHAMMED MATUMLA KATIKA POZI
FRANCISE MIYEYUSHO KUSHOTO AKIWA NA MOH'D MATUMLA KATIKA PICHA YA PAMOJA.
MABONDIA HAO WAKITAMBIANA WAKITAMBIANA, PEMBENI KULIA  NA ALIYEVAA KAPELO NYEUSI  BONDIA WA ZAMANI RASHID MATUMLA AMBAYE PIA NI BABA MZAZI WA MOHD MATUMLA.

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK