MUSOMA:
MAANDALIZI
YA KUZIMA MITAMBO YA ANALOJIA YA UTANGAZAJI WA TELEVISION KWA MJI WA MUSOMA
MKOANI MARA YAMEKAMILIKA KWA KUWASHIRIKISHA WADAU WA SEKTA YA UTANGAZAJI.
AWAMU
HII INAHUSISHA MIKOA YA MARA NA KAGERA NA HII NI BAADA YA ZOEZI HILO KUKAMILIKA KATIKA
MIKOA YA SINGIDA NA TABORA
MITAMBO
ITAZIMWA SAA SITA KAMILI USIKU WA TAREHE 30 APRIL, 2014 HUKU KUWEPO UTANGAZAJI
WA MFUMO WA ANALOJIA PAMOJA NA KIDIJITI KWENYE ENEO HUSIKA, UPATIKANAJI
VINGAMUZI NA UWEPO WA CHANELI TANO ZA KITAIFA KWENYE MFUMO WA KIDIJITI
VIKITUMIKA KAMA VIGEZO VYA ZOEZI HILO.
MENEJA
MAWASILIANO WA MAMLAKA YA MAWASILIANO NCHINI (TCRA) BW INNOCENT MUNGY AMEELEZA
KUWA MAENEO AMBAYO HAYANA MIUNDO MBINU YA DIJITALI HAYATAZIMWA KWASASA HADI
YAPATE DIJITALI HUKU AKISISITIZA KUWA MABADILIKO HAYO HAYAHUSU MATANGAZO KWA
NJIA YA UTANGAZAJI WA SATELAITI, WAYA (CABLE) NA REDIO.
ZOEZI
HILO LINAKUJA HUKU KUKIWA NA CHANGAMOTO YA GHARAMA ZA VINGAMUZI AMBAPO WANANCHI
HASA WAKIPATO CHA CHINI WAKISHINDWA KUMUDU KUNUNUA NA KULIPIA VIFURUSHI VYA
KILA MWEZI
AIDHA
MAMLAKA YA MAWASILIANO (TCRA) IMEAGIZA WATOA HUDUMA ZA KUSAMBAZA VINGAMUZI
WALIOKO MJINI MUSOMA KUHAKIKISHA KUWA KUNAKUWA NA VINGAMUZI VYA KUTOSHA.
MWISHO........
0 comments:
Post a Comment