`

Home » » KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI MUSOMA CHA VUNJWA...BOFYA HAPA USOME

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI MUSOMA CHA VUNJWA...BOFYA HAPA USOME

MUSOMA.

MADIWANI WA MANISPAA YA MUSOMA LEO WAMEAHIRISHA BARAZA AMBALO NI MWENDELEZO WA SHUGHULI ZA BARAZA KWA MUJIBU WA KANUNI KWA LENGO LA KUWASILISHA TAARIFA ZA KATA KUTOKANA NA MAKOSA YALIYOFANYWA NA OFISI YA MKURUGENZI KUSHINDWA KUTOA TAARIFA KWA MADIWANI NA WATENDAJI WA KATA.

AKIZUNGUMZA NA VICTORIA FM DIWANI WA MAKOKO KUPITIA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO CHADEMA BW. ALOYCE RENATUS AMESEMA KUWA KIKAO HICHO AWALI KILITAKIWA KUANZA KWA MADIWANI AMBAO NDIYO WENYEVITI WA WDC KUTAKIWA KUWASILISHA TAARIFA ZA KATA, NA KUFUATIWA NA KIKAO CHA KILA DIWANI KUKAA KIKAO CHA KICHAMA NA MWISHO NDIPO KIENDELEE KIKAO CHA MADIWANI CHA KAWAIDA.


NAYE DIWANI WA KATA YA KAMNYONGE BI. ANGELA DERICK LIMA AMEMUOMBA MKURUGENZI KUMUOMBA MKURUGENZI AWAOMBE RADHI NA KUANDAA UPYA BARAZA HILO KWA GHARAMA ZAKE ILI KUHAKIKISHA TARATIBU ZOTE ZINAFANYIKA.


BAADA YA KUAHIRISHWA KWA BARAZA HILO MAKAMU MWENYEKITI AKATOA MUONGOZO ULIOTOLEWA NA SERIKALI UNAOTAKA MABARAZA YA HALMASHAURI KUFANYA SEMINA YA PAMOJA KATI YA MADIWANI NA WATENDAJI WA KATA YA NAMNA YA KUNDAA TAARIFA AMBAPO SEMINA HIYO ITANYIKA MAY 7 NA 8.

AIDHA AMEONGEZA AMEWATAKA WATENDAJI KATA KUKAA KIKAO WAKIANZIA SIKU YA IJUMAA ILI KUANDAA TAARIFA SIKU YA JUMATATU AMBAPO VIONGOZI WA KATA KILA MMOJA KUKAA NA KUZIPITIA TAARIFA ZAKE SIKU YA JUMATATU NA KABLA YA KUZIFIKISHA KUZIFIKISHA KWENYE KATA (WDC) NA BAADAE KUINGIZWA KWENYE BARAZA SIKU YA JUMANNE NA SIKU YA JUMAATANO AMBAPO BARAZA LINGINE LITAKAPOKAA ILI KUPITIA KAMATI ZA KUDUMU PAMOJA NA MAMBO MENGINE NA HII NI KUTOKANA NA MWONGOZO WA SERIKALI KUTAKA VIKAO VYA BARAZA YA HALMASHAURI KUKALIWA MARA TATU.


HATA HIVYO KAIMU MKURUGENZI WA MANISPAA AMESEMA KUWA ILI KIKAO KIKALIWE AU KISIKALIWE NI WAZI KUWA WAJUMBE WANATAKIWA KUKUBALIANA HUKU MAAMUZI YAKIFANYWA NA MWENYEKITI AU MAKAMU MWENYEKITI


0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK