NDOTO ya tanzania kufanya vyema katika mchezo wa ya madola kwa upande wa masumbwi imeanza vibaya baada ya nahodha wa timu ya taifa ya tanzania kwa upande wa masumbwi Selemani Kidunda kupoteza mchezo wake dhidi ya bondia kutoka nchini Nigeria Kehinde Ademuyiyiwa katika pambano la uzito wa kilo 69 na hivyo kupoteza nafasi ya kusonga katika hatua inayofuata katika michezo ya jumuiya ya Madola inayofanyika Glasgow nchini Scotland.
Akiongea na mtandao wa chanzo cha habari hii kocha mzalendo wa timu ya ngumi John Mwakipesile amesema mchezo ulikuwa ni mzuri kwa upende wa Kidunda kwa roundi zote tatu za mchezo na mpaka kufikia mwisho walikuwa wakijua Kidunda ameshinda lakini ikawa ni ajabu kwa watu wengi kutangazwa Ademuyiyiwa kuwa ndiye mshindi.
Amesema mpinzani wake alikuwa akitumia mbinu chafu ya kumpiga vichwa Kidunda katika sehemu kubwa ya mchezo huo kitu ambacho waamuzi wa mchezo walikuwa wakikiona na kushindwa kukemea hilo.
Kuondolewa kwa Kidunda ni pigo kubwa kwa Tanzania ambayo ilikuwa imeweka matumaini makubwa kwa nahodha huyo wa Tanzania katika michezo hiyo ya Madola.
Kesho bondia mwingine Nasser Mafuru anataraji kupanda ulingoni kucheza dhidi ya Jessie Lartey wa Ghana huku bondia mtanzania Mafuru akitamba kumchapa mpinzani wake huyo.
NAHODHA SULEIMAN KIDUNDA PIACHANI
0 comments:
Post a Comment