WAZIRI WA MAENDELEO JINSIA NA WATO MHE SOFIA SIMBA AMEIKUMBUSHA JAMII KUWA SUALA LA KULEA WATOTO NI JUKUMU LA WAZAZI WENYEWE NA KUITAKA JAMII KUZINGATIA MALEZI BORA KWA WATOTO WAO.
WAZIRI SIMBA AMESEMA HAYO KWA NYAKATI TOFAUTI MJINI MUSOMA WAKATI AKIONGEA NA WANANCHI WA KATA ZA BWERI NA MWISENGE AMBAO AMEIKUMBUSHA JAMII UMUHIMU WA SUALA ZIMA LA ELIMU KWA WATOTO WAO IKIWA NI PAMOJA NA WAZAZI KUKAA PAMOJA NA WATOTO KUWAELIMISHA JUU YA MADHARA YA NDOA ZA UTOTONI KWA WATOTO WA KIKE.
PIA WAZIRI SIMBA AMESISITIZA WAZAZI, WALEZI PAMOJA NA WALIMU KUTOWANYANYAPAA NA KUTOA ADHABU KALI KWA WATOTO WAO BADALE YAKE AMEWATAKA KUDUMISHA UPENDO ILI KUEPUSHA KUJENGA CHUKI KATI YAO NA WATOTO HUKU AKISISITIZA KUWA ATAKAYEBAINIKA AKIMNYANYASA MTOTO ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA.
MWISHO
MWENYEKITI CWT AMABAYE PIA NI WAZIRI WA WAZIRI WA MAENDELEO JINSIA NA WATOTO AKIWA NA AKINA MAMA MKOANI MARA.
0 comments:
Post a Comment