NA AHMAD NANDONDE,
MUSOMA.
WAKAZI WA KATA
YA KIGERA WAMEOMBWA KUWAHAMASISHA WANANCHI WAISHIO MANISPAA YA MUSOMA
KUJITOKEZA KWA WINGI KWAAJILI YA KUWAPELEKA WATOTO WAO KATIKA ZOEZI LA
UPATIWAJI CHANJO YA SURUA RUBELA NA MINYOO.
HAYO YAMESEMWA
NA KATIBU TAWALA WILAYA YA MUSOMA BW. HASHIM MGONJA ALIPOKUWA AKIZINDUA ZOEZI
LA UPATIWAJI CHANJO HIYO JANA KATIKA KITUO CHA AFYA CHA KWANGWA KILICHOPO
MANISPAA YA MUSOMA.
BW. MGONJA
AMESEMA KUTOKANA NA KUGUNDULIKA KWA MARADHI HAYO NI WAZI KUWA KILA MWANANCHI
ANATAKIWA KUWAHAMASISHA WENZAO ILI KUWAPELEKA WATOTO KATIKA VITUO VYA AFYA
KWAAJILI YA KUPATIWA CHANJO HIYO.
NAYE KAIMU
MGANGA MKUU WA MANISPAA YA BW KITWALE MAKWE AMESEMA ZOEZI HILO LA KITAIFA
LIMEANZA OCT. 18 NA LINATARAJI KUMALIZIKA OCT. 24 KATIKA MANISPAA NZIMA YA
MUSOMA LIKIWA NA LENGO LA KUWAKINGA WATOTO NA MAGONJWA YA SURUA RUBELA, MINYOO
KUHARA NA UPUNGUFU WA DAMU.
AKISOMA RISALA
KWA MGENI RASMI MUUGUZI WA KITUO CHA AFYA CHA KWANGWA BI. REHEMA JUMA AMESEMA
WATOTO 72,711 WA MANISPAA YA MUSOMA WAMEANZA KUPATIWA CHANZO HIYO KATIKA
ZAHANATI, VITUO VYA AFYA, SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZILIZOPO KATIKA MAENEO
HUSIKA.
CHANJO YA SURUA
RUBELA INALENGA KUWASIDIA WATOTO WALIOCHINI YA MIEZI 9 HADI MIAKA 14, VITAMIN A
KWA WATOTO WENYE UMRI WA KUANZIA MIEZI 6
HADI MIEZI 59 PAMOJA NA DAWA YA KUUA MINYOO KWA WATOTO WENYE UMRI KUANZIA MWAKA
MMOJA HADI MIAKA MITANO.
ZOEZI HILO
AMBALO LINATOLEWA BURE KWA KILA MTOTO LIMEBEBA UJUMBE UNAOSEMA UTOAJI WA CHANJO
HIYO NI “LINDA MAISHA, OKOA MAISHA ZUIA ULEMAVU- KAMILISHA CHANJO”.
MWISHO....
0 comments:
Post a Comment