Home »
» ULINZI WAIMARISHWA MARA DUFU NI KATIKA USIKU WA AFTER SCHOOL GET TOGETHER PARTY.
ULINZI WAIMARISHWA MARA DUFU NI KATIKA USIKU WA AFTER SCHOOL GET TOGETHER PARTY.
Na Ahmad Nandonde,
Musoma.
Wakati show kubwa na ya kiburudani iliyopewa jina la after skonga get together party ikitarajiwa kufanyika siku ya jumamosi ulinzi umezingatiwa kwa kiasi kikubwa ili kuhakikisha watazamanji wanaondokana na bughudha toka kwa watu wenye nia mbaya.
Hayo amesemwa na mratibu wa show hiyo Bw. Patrick Mwakale alipokuwa akizungumza na kipindi cha zig zaga la michezo kinachorushwa na radio victoria fm kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa kumi na moja kamili jioni.
Amesema kwa hivi sasa kila kitu kinakwenda kama kilivyopangwa huku akigusia katika suala la ulinzi na usalama katika tukio hilo kubwa siku ya jumamosi Bw. Mwankale alisema kuwa mkoa wa Mara ni miongoni mwa mikoa nayokabiliwa na wimbi kubwa la uvunjifu wa amani hivyo ili kuhakikisha hilo halitokea katika usiku huo ameahidi kuhakikisha analisimamia ipasavyo kwa kulishirikisha jeshi la polisi mkoani hapa na hata ulinzi shirikishi.
“Kiukweli hakuna kati yetu asiyejua kama mkoa wetu unakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa amani hivyo ili kuhakikisha hilo halitokea katika usiku huo na ninaahidi kulisimamia ipasavyo kwa kulishirikisha jeshi la polisi mkoani hapa na hata watu wa ulinzi shirikishi ili kuondokana na kero zozote zile zitakazojitokeza siku hiyo”.alisema…….
Jumla ya watazamaji 3,500 wanataraji kuhudhuria katika tukio hilo la kihistoria na la aina yake ambalo linaelezwa kuwa la kwanza katika macho na masikio ya wakazi wa manispaa ya Musoma huku lengo kuu likiwa ni kuwakutanisha wahitimu mbali mbali wa shule za sekondari na hata vyuo katika kipindi cha mwaka 2013.
Aidha Mwankale aliwaomba wakazi wa mkoa wa mara na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi na hii ni kutokana na kuwepo kwa maandalizi makubwa zurina ya kipekee ambayo hayajawahi kufanyika katika manispaa ya musoma.
“Kutokana na maandalizi mazuri na mambo matamu niliyoyaandaa kwa mimi sidhani kama kutakuwa na sababu ya mtu kukosa ndo maana nawaomba wana mara na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi ili tufurahi na wadogo zetu kwa pamoja show hiyo”. alimalizia.….
Show hiyo inayotaraji kufanyika katika ukumbi wa bwalo la magereza nov. 30 siku ya Jumamosi itapambwa na wakali kibao watakaokonga nyoyo za wahudhuriaji ni pamoja na Jazz Bee, Spea Boy, B.R Kizzo a.k.a Isaya, Abbibaro, Jax Flax, bila kuwasahau Musoma Dancer’s na wengine kibao.
Tayari tiket zinapatikana “Man D” hair cutting saloon iiyopo majita road ulizia Dotto, Mara high school pale ulizia Jax Flax , Bwalo la magereza ulizia kaunta, “Kiss B” barber shop na Radio Victoria Fm iliyopo maeneo ya kwangwa manispaa ya musoma na hapo utaulizia Moses.
Mwisho…..ULINZI WAIMARISHWA MARA DUFU NI KATIKA USIKU WA AFTER SCHOOL GET TOGETHER PARTY.
0 comments:
Post a Comment