`

Home » » WOMEN JAZZ BAND NI BANDI YA WANAWAKE NI BENDI ILIYOWAHI KUTAMBA MWAKA 1966.

WOMEN JAZZ BAND NI BANDI YA WANAWAKE NI BENDI ILIYOWAHI KUTAMBA MWAKA 1966.


WOMEN JAZZ BAND NI BANDI YA WANAWAKEbendi ya akina mama 1966.

Kijakazi Mbegu kwenye solo gitaa

Mwaka 1965 kundi jipya la muziki la aina yake lilianzishwa Tanzania. Lilikuwa ni bendi ya akina mama watupu.

Akina mama hawa, wengine wakiwa wafanya kazi wa Government Press walijichagua na kuanza kuhudhuria mafunzo ya muziki chini ya yule mwanamuziki mahiri Mzee Mayagilo aliyekuwa kiongozi wa shughuli za muziki katika Jeshi la Polisi.

Akina mama hawa wakawa chini ya kitengo cha Polisi Jazz Band, wakaanza kufanya mazoezi ya nguvu.

Bendi hiyo ya akina mama ilikuwa chini ya TANU Youth League. Wakati wakianza shughuli hii walikuwa hawana ujuzi wowote wa muziki.

Kutokana na jitihada waliyofanya taratibu wakaanza kufanya maonyesho yao hasa kwenye hafla za serikali na Chama tawala wakati huo.

Tarehe 31 Mei 1966 Women Jazz band iliingia katika studio za RTD na kurekodi nyimbo sita.

1. Tumsifu Mheshimiwa

2. Leo Tunafuraha

3.Mwalimu Kasema

4.Women Jazz

5.Sifa nyingi tuwasifu viongozi

6.TANU yajenge nchi.

Washiriki katika bendi hiyo walikuwa;
1.Mary Kilima- Mwimbaji

2.Juanita Mwegoha-Mwimbaji

3.Siwema Salum- Mwimbaji

4.Rukia Hassan- Mwimbaji

5. Kijakazi Mbegu- Solo Guitar

6.Mwanjaa Ramadhan-Bass Guitar

7.Chano Mohammed-Rhythm Guitar

8.Tatu Ally-Alto Sax

9.Mina Tumaini-Tenor Sax

10. Anna Stewart-Alto Sax

11. Rukia Mbaraka-Tenor Sax

12.Lea Samweli-Bongos

13. Josephine James-Drums

14. Zainab Mbwana-Maracass

15. Tale Mgongo-Timing.

Women Jazz ilipata umaarufu kiasi cha kuanza kufanya safari nje ya Tanzania, na kuweza kufanya maonyesho Nairobi na Mombasa, baada ya kutembelea miji kadhaa hapa nchini.

Wakati wa matayarisho ya kwenda China kundi lilisambaratika. Kikubwa kilichosababisha hili ilikuwa ni wanamuziki kuona hawapati chochote kutokana na mapato yaliyotokana na muziki.

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK