`

Home » » LUNYAMILA HALI YA KIAFYA SI SHWARI SASA APUMULIA MIPIRANI BAADA YA KUBANWA NA KIFUA.

LUNYAMILA HALI YA KIAFYA SI SHWARI SASA APUMULIA MIPIRANI BAADA YA KUBANWA NA KIFUA.

WINGA wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, Edibily Lunyamila leo hii asubuhi amekimbizwa katika hospitali ya Mwananyamala baada ya kusumbuliwa na kifua na sasa anapumua kwa msaada wa mashine. Tulifanikiwa kufika hospitalini hapo muda mfupi baada ya winga huyo kukimbizwa hospitalini hapo baada ya kuzidiwa tangu jana usiku akiwa nyumbani kwake Mbezi jijini Dar es Salaam.

Tulimshuhudia Lunyamila akiwa amelala kitandani katika wodi ya wanaume namba namba 5 kitanda namba 16 katika hospitali hiyo ya rufaa ya Kinondoni. Daktari Madirisha Pascal anayemuhudumia winga huyo wa zamani, Lunyamila anasumbuliwa na tatizo la kifua ambalo linamfanya ashindwe kupumua vizuri.

“Kama mnavyomuona anapumua kwa msaada wa mashine na bado tunaendelea kumfanyia uchunguzi ili kubaini nini kinachomsumbua zaidi,” alisema DR. Pascal.

Mmoja wa ndugu wa Lunyamila, Lameck John alisema kwamba, mchezaji huyo wa zamani alianza kujisikia vibaya jana Jumapili na leo asubuhi hali yake ilibadilika ndipo walipomkimbiza hospitali.

“Alianza kulalamika hawezi kupumua na kifua kinamsumbua pia mbavu zilikuwa zikimuuma, baada ya majibu ya vipimo tutajua kinachomsumbua zaidi,” alisema Lameck.

Kutokana na hali iliyoonekana hospitalini hapo, Lunyamila anahitaji huduma ya haraka ili kuweza kuokoa uhai wake kwani anapumulia mashine akiwa katika sehemu yenye joto kali hivyo anapambana na vitu vingi kwa wakati mmoja. Taarifa za kiuchunguzi zilizofanywa zimebaini Lunyamila anasumbuliwa na ugonjwa wa moyo.

''Nilikuja jana hospitali ya mwananyaala ikagundulika moyo wangu umekuwa mkubwa,hivi sasa naenda muhimbili kwa ajili ya vipimo zaidi nikifika na kukutana na daktari nitakujulisha ''
Lakini ilipofika mchana wa leo mwandishi alipokea simu kutoka kwa Lunyamila akimwambia ameambiwa arejee tena hospitali ya Mwananyamala.

MTAKIE AFYA NYEMA MCHEZAJI ALIYEITUMIKIA NCHI YAKE KWA MOYO WAKE WOTE. WAGANDA HAWATAMSAHAU ALICHOWAFANYA MWAKA 1993 KOMBE LA KAGAME (WAKATI HUO HALIKUITWA KAGAME BALI KLABU BINGWA AFRIKA MASHARIKI NA KATI)

CHANZO:FANS SIMBA NA YANGA

FANS:SIMBA NA YANGA

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK