Home »
» UHARIBIFU WA MIUNDO MBINU YA BARABARA CHANZO KIKUBWA NI NG'OMBE NA MBUZI.
UHARIBIFU WA MIUNDO MBINU YA BARABARA CHANZO KIKUBWA NI NG'OMBE NA MBUZI.
Na Bosco Robert,
Butiama.
Imeelezwa kuwa uharibifu wa miundo mbinu ya barabara pamoja na miundo mbinu ya maji umekuwa ukichangiwa na mifugo kama ngombe na mbuzi pindi inapopitishwa katika miundo mbinu hiyo.
Hayo yasemwa na wakazi wa vijiji vya kwikuba na maneke vilivyopo wilayani butiama walipokuwa wakizungumza na blog ya jicho la mdadisi hapo jana katika semina ya utunzanji wa vyanzo vya maji vijijini kufuatia uhaba wa maji uliovikumba vijiji hivyo kwa muda mrefu hivi sasa.
Aidha wakazi hao wameongeza kuwa upitishaji wa mifugo hiyo kumesababisha momonyoko mkubwa wa udongo pembezoni mwa barabara kulikopelekea uharibifu wa mitaro ya barabara na kufanya vyombo vya usafiri kupita kwa shida.
Katika kuthibitisha hilo wakazi hao wametolea mfano barabara itokayo musoma kuelekea majita kijiji cha kwa namna ilivyoharibika ikiwa ni pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji kama vile visima, na mabwawa, mifereji baada ya wafugaji kupitisha mifugo yao pindi wanapowapelekea machungani.
Kwa upande mwingine wakazi hao wameiambia blog ya jicho la mdadisi kuwa kuwa ajali nyingi zinazotokea katika barabara hiyo zinachangiwa na upitishaji wa mifugo hiyo ambapo zaidin ya ajali mbili hadi tatu zimekuwa zikiripotiwa kwa siku moja.
Aidha kwa upande wa wafugaji hao wameiomba serikali kuwatengea maeneo maalumu vijini humo kwa aajili ya malisho ya mifugo yao ili kuepusha kero na migogoro dhidi yao na wakulima jambo ambalo linaweza kupelekea nchi kuingia katika dimbwi la machafuko baina ya wakulima na wafugaji.
Mwisho………………
0 comments:
Post a Comment