RORYA
MCHUNGAJI WA KANISA LA APOSTOLIC LILILOKO MJI MDOGO WA SHIRATI
WILAYANI RORYA, MKOA WA MARA, AMEUAWA NA WATU WANAOSADIKIWA KUWA MAJAMBAZI KWA
KUPIGWA RISASI USIKU WA KUAMKIA JANA.
HATA HIVYO, KAMANDA WA JESHI LA POLISI KANDA MAALUMU YA
TARIME/RORYA, JUSTUS KAMUGISHA LICHA YA KUKIRI KUTOKEA KWA TUKIO HILO, ALISEMA
POLISI WANAENDELEA NA UCHUNGUZI.
HABARI ZILIZOPATIKANA KUTOKA KATIKA ENEO LA TUKIO, ZINASEMA MCHUNGAJI HUYO, OWITI ARIRI ALIUAWA MUDA MFUPI BAADA YA KUKABIDHIWA SANDUKU LA FEDHA ZA KIKUNDI CHAO CHA KUWEKA NA KUKOPA ALICHOKUWA AKIKIFANYIA KAMA MWEKA HAZINA.
HABARI ZILIZOTHIBITISHWA NA MCHUNGAJI MWENZAKE, CHRISTOPHER NYAITEGA, ZINASEMA TUKIO HILO LILITOKEA JUZI KATIKA MOJA YA HOTELI ILIYOKO KATIKA MJI HUO.
MCHUNGAJI NYAITEGA AMBAYE HATA HIVYO HAKUWEZA KUJUA KIASI CHA FEDHA KILICHOKUWEMO NDANI YA SANDUKU HILO KWA KUWA YEYE SIYO MMOJA WA WANAKIKUNDI, ALISEMA WANAKIKUNDI WALIAMUA KUMKABIDHI FEDHA HIZO ILI AZIPELEKE BENKI KESHO YAKE.
AMESEMA AKIWA NYUMBANI KWAKE, ALIFIKIWA NA MMOJA WA WANAKIKUNDI WENZAKE ALIYEANZA KUDADISI KUHUSU FEDHA HIZO, AMBAPO MAREHEMU ALIMHAKIKISHIA KUWA ZIKO SALAMA HALI ILIYOMFANYA MGENI WAKE HUYO AONDOKE.
AMESEMA MUDA MFUPI BAADA YA MGENI HUYO KUONDOKA, GHAFLA MAJAMBAZI WALIFIKA NYUMBANI HAPO NA KUMTAKA MAREHEMU AWAPE FEDHA HIZO KABLA YA KUMUUA.
AMESEMA JESHI HILO LINAMSHIKILIA MWANAKIKUNDI HUYO KWA MAHOJIANO ZAIDI, HUKU AKIAHIDI KUTOA TAARIFA ZAIDI KUHUSIANA NA TUKIO HILO LEO.

0 comments:
Post a Comment