Home »
» MAWAZIRI WATATU WAJIUZULU NCHINI UTUIRUKI.
MAWAZIRI WATATU WAJIUZULU NCHINI UTUIRUKI.
Moscow.
Mawaziri watatu nchini Uturuki wamejiuzulu leo, siku chache baada ya watoto wao wa kiume kukamatwa kufuatia kashfa kubwa ya ufisadi ambayo imewalenga washirika wa Waziri Mkuu Recip Tayyip Erdogan katika mojawapo ya migogoro mikubwa zaidi kuwahi kuukumba uongozi wake wa zaidi ya miaka kumi.
Waziri wa Uchumi Zafer Caglayan na Waziri wa Mambo ya Ndani Muammar Guler wametangaza kujiuzulu kwao katika taarifa zilizotolewa na shirika la habari la serikali la Anadolu.
Waziri wa Mazingira na Mipango ya Maeneo ya mijini Erdogan Bayraktar naye ametangaza kujiuzulu kutoka serikalini na bungeni katika mahojiano na kituo cha kibinafsi cha televisheni NTV ana kumtaka pia Waziri mkuu kujiuzulu.
Mawaziri wote watatu wamekanusha kufanya makosa yoyote.
Watoto wa Caglyan na Guler, pamoja na Afisa Mkuu Mtendaji wa benki ya serikali Halkbank, ni miongoni mwa watu 24 waliokamatwa kwa tuhuma za rushwa.
Polisi walipata dola milioni 4.5 pesa taslimu katika masanduku ya viatu nyumbani kwa Mkuu huyo wa benki, huku nyingine milioni moja zikigundulika nyumbani kwa mwanawe Guler.
Chanzo: DW
0 comments:
Post a Comment