Home »
» MKWASA HAENDI YANGA NG'OOO. "MASAU"
MKWASA HAENDI YANGA NG'OOO. "MASAU"
Klabu ya soka ya ruvu shooting leo imekanusha vikali taarifa zilizozagaa kuwa kocha wao charles boniface mkwasa amesaini mkataba na klabu ya yanga.
Akizungumza na blog ya jicho la mdadisi hii leo msemaji wa klabu ya ruvu shooting amekanusha vikali taarifa hizo huku akiziita ni za uongo na wala kocha huyo hatong'oka hapo wala hana mpango huo.
Akitilia msisitizo juu ya kutoondoka kwa kocha huyo masau amesema kitendo cha kauli hiyo ambayo si rasmi ni cha uongo na kama yanga wanampango huo basi wanajidanganya pamoja na kuwadanganya mashabiki wao.
Charles Boniface Mkwasa ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya yanga miaka ya themanini alikuwani mmoja wachezaji wenye nidhamu ya hali ya juu kabisa ikilinganishwa hata na kiwango chake pale alipokuwa uwanjani.
Enzi za uchezaji wake mkwasa ni alikuwa ni mchezaji ambaye hakuwahi kupewa kadi yeyote kwamaana kuwa si kadi ya njano wala nyekundu.
Mkwasa amewahi pia kuzifunda timu mbali mbali ikiwemo timu ya taifa kwa vipindi tofauti katika miaka ya 90 na 2000 lakini pia amewahi kuifunda timu yake ya zamani ya yanga, timu ya taifa ya wanawake hivi sasa ndiye kocha mkuu wa klabu ya ruvu shooting inayomilikiwa na jeshi la kujenga taifa lenye maskani yake huko kibaha mlandizi mkoani pwani.
Kocha sir Boniface Mkwasa
Masau Bwire Msemaji Ruvu Shooting
0 comments:
Post a Comment