`

Home » » SACCOS MARA CHATARAJI KUWEKEZA ZAIDI KATIKA MIRADI MIKUBWA YA KIMAENDELEO.

SACCOS MARA CHATARAJI KUWEKEZA ZAIDI KATIKA MIRADI MIKUBWA YA KIMAENDELEO.

Na Ahmad Nandonde,

MUSOMA.

CHAMA CHA AKIBA NA MIKOPO MKOANI MARA IMARA SACCOS KINATARAJIA KUWEKEZA ZAIDI KATIKA MIRADI MBALIMBALI ILI KULETA MAENDELEO KATIKA JAMII.

HAYO YEMSEMWA JANA NA MWENYEKITI WA BODI YA CHAMA CHA USHIRIKA WA AKIBA NA MIKOPO (IMARA SACCOS) BW. BONIFACE NDENGO KATIKA MKUTANO MKUU WA CHAMA HICHO ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA MUSOMA KLABU ULIOPO KATIKA MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA.

BW. NDENGO AMESEMA KUWA HIVI SASA WAMEAMUA KUJIKITA ZAIDI KATIKA UWEKEZAJI WA MIRADI MIKUBWA KAMA BANK IATAKAYOSAIDIA WAJASILIA MALI KUPATA MIKOPO, MIRADI YA ELIMU ITAYOSAIDIA WANACHAMA KUSOMESHA WATOTO WAO KWA GHARAMA NAFUU IKIWA PAMOJA NA MIUNDO MBINU KWA KUBORESHA BARABARA KWA KIWANGO CHA LAMI.


AIDHA NDENGO AMEZITAJA BAADHI YA CHANGAMOTO WANAZOKABILIANA NAZO KUWA NI PAMOJA NA WANACHAMA WENGI KUTOKUWA NA UELEWA KATIKA DHANA YA UWEKEZAJI, WATU KUTOSHIRIKI KATIKA FURSA MBALI MBALI NA HII NI KUTOKANA NA BAADHI YA WATU KUKATA TAMAA HALI INAYOPELEKEA KUAMUA KUTOA ELIMU YA KUTOSHA KWA WANACHAMA WAO.


HATA HIVYO AMETOA WITO KWA WANANCHI MKOANI HAPA KUJIUNGA NA CHAMA HICHO ILI KUWEKEZA KATIKA MIRADI MIKUBWA ILI KUBADILISHA HALI ZA KIMAISHA KIUCHUMI NA HATA KIJAMII.

1 comments:

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK