Story na Ahmad Nandonde,
Musoma.
MFANYABIASHARA MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA GEOFREY GUNDURA MKAZI WA BUHARE MGARANJABO MANISPAA YA MUSOMA MKOANI MARA AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUPIGWA RISASI NA WATU WANAODHANIWA KUWA NI MAJAMBAZI ALIPOKUWA NYUMBANI KWAKE.
AKITHIBITISHA KUTOKEA KWA TUKIO HILO KAMANDA WA JESHI LA POLISI MKOANI MARA SACP. FERDINAND MTUI AMESEMA TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 15 MWEZI HUU BAADA YA MAJAMBAZI HAO KUVAMIA NYUMBANI KWA MAREHEMU NA KISHA KUMPIGA RISASI KWENYE UBAVU WA KUSHOTO NA HIVYO KUSABABISHA KIFO CHAKE.
KAMANDA MTUI AMESEMA MBALI NA MAJAMBAZI HAO KUFANYA TUKIO HILO WALIFANIKIWA PIA KUPORA MALI ZA MAREHEMU ZIKIWEMO SIMU MBILI ZA MKONONI PAMOJA NA FEDHA TASLIMU SHILINGI LAKI NNE.
KUFUATIA TUKIO HILO JESHI HILO LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA KUHUSIKA NA TUKIO HILO.
HATA HIVYO KAMANDA MTUI METOA WITO KWA WANANCHI MKOANI HAPA KUSHIRIKIANA NA JESHI HILO KATIKA UTOAJI WA TAARIFA ZA SIRI ZITAKAZOWEZA KUPATIKANA KWA WATU HAO ILI SHERIA IWEZE KUCHUKUA MKONDO WAKE.
MWISHOOO.........
Home »
» MFANYABIASHARA MKOANI MARA AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA MAJAMBAZI.
0 comments:
Post a Comment