`

Home » » SERIKALI MKOANI MARA YAWAPONGEZA WADAU WA KILIMO.

SERIKALI MKOANI MARA YAWAPONGEZA WADAU WA KILIMO.

Na Pendo Mwakyembe.

MUSOMA.

HALMASHAURI NA WADAU WA KILIMO MKOANI MARA WAMEPONGEZWA KWA KUFANYA KAZI NZURI YA KUENDELEZA KILIMO CHINI YA MRADI WA DASIP KUFUATIA MABADILIKO CHANYA YA MIUNDO MBINU MBALIMBALI YA KILIMO NA TEKNOLOJIA ZA KILIMO KATIKA MAENEO YALIYOPITIAWA NA MRADI.


AKITOA PONGEZI HIZO KWANIABA YA MKUU WA MKOA MKUU WA WILAYA YA RORYA BW. ELIAS GOROI AMESEMA KUWA HALMASHAURI ZOTE TANO ZINAZOTEKELEZWA DASIP KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI ZIMETEKELEZA MIRADI 503 AMBAPO KATI YA MIRADI HIYO MIRADI 429 TAYARI IMEKAMILIKA HUKU MIRADI 373 IKIELEZWA KUWA NDIYO INAYOTUMIKA KWA HIVI SASA.


PIA AMETUMIA FURSA HIYO KUWAHIMIZA KUTAFAKARI MAMBO MAZURI YALIYOFANYWA NA MRADI NA CHANGAMOTO ZILIZOPO NA JINSI YA KUZIONDOA.


AMESEMA DASIP HIVI SASA IMEJIJENGEA UWEZO WA KWA KUTOA MAFUNZO YANAYOHUSU MFUMO WA MASOKO YA KILIMO KWA WATAALAM KATIKA NGAZI YA MKOA NA WILAYA 5 PAMOJA NA HALMASHAURI TANO ZINAZOTEKELEZA MRADI HUO.

MBALI NA MAFUNZO HAYO PIA DASIP TAYARI IMESHATOA MAFUNZO KWA WATAALAM NA VIONGOZI WA NGAZI YA MIKOA, WILAYA, KATA NA HATA VYAMA VYA AKIBA NA KUKOPA 15 VINAVYOJULIKANA KAMA SACCOS IKIWA NI PAMOJA NA UBORESHAJI WA HUDUMA ZA FEDHA VIJIJINI KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI.

WARSHA HIYO YA UENDELEZAJI WA MASOKO YA BIDHAA ZA KILIMO IMEFANYIKA HII LEO MJINI MUSOMA KATIKA UKUMBI WA UWEKEZAJI ULIOPO KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA MARA. 


0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK