`

Home » » POLISI MORO YAKAMATA WATATU NA MWILI WA MAREHEMU WENYE MADAWA YA KULEVYA.

POLISI MORO YAKAMATA WATATU NA MWILI WA MAREHEMU WENYE MADAWA YA KULEVYA.

Morogoro.

Jeshi la polisi mkoani morogoro limefanikiwa kukamata gari dogo aina ya toyota spacio likiwa limebeba mwili wa marehemu khalid kitala (47) ukiwa na kete kadhaa za madawa ya kulevywa tumboni.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa jeshi la polisi mkoani morogoro, faustine shilogile amesema jeshi la polisi lilipokea taarifa hizo toka kwa wasamaria wema juu kuwepo kwa gari hilo njiani likitokea mkoani mbeya kuelekea dar es salaam.

Mara baada ya kupatia taarifa hizo polisi waliweka mtego kwenye kituo cha mikumi na hatimaye kufanikiwa kulikamata gari hilo likiwa na watu watatu ndani (majina yao yamehifadhiwa), vitu vlivyofungwa mithili ya pipi saba vinavyosadikiwa kuwa ni dawa za kulevya.

Baada ya polisi kukamata gari hilo waliuchukua mwili wa marehemu na kisha kuupeleka hospitali kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi na kufanikiwa kukuta pipi nyingine kumi na saba tumboni mwa marehmu huyo ambaye inasemekana alifariki akiwa jijini mbeya.

Watu hao watatu ambao wawili kati yao ni wahusika wa gari hilo na mmoja ni mfanyabiashara kariakoo jijini dar es salaam wanashikiliwa na polisi mkoni morogoro kwa uchunguzi zaidi.

Mwishooo......

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK