Iringa.
Mkuu wa mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma,amewataka wafanyabiashara mkoani Iringa kuacha kupandisha bei ya vyakula katika kipindi hiki cha sikukuu ya krismasi na mwaka mpya, na kutoa onyo kwa atakayekiuka kuwa atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Dk.ishengoma ameema hayo alipokuwa akitoa salamu za krismasi na kuwatakia heri ya mwaka mpya wakazi wa mkoa wa iringa mbele ya waandishi wa habari jana huku akitoa agizo kwa wakurugenzi wa halmashauri zote za wilaya kuzunguka mitaani kuchunguza bei ya bidhaa na kuwachukulia hatua wanaopandisha bei kiholela.
Amesema imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya wafanyabiashara kutumia sikukuu mbalimbali kujipatia fedha kwa kuwanyonya wananchi,jambo ambalo halitovumiliwa mkoani humo.
Amesema lengo la kuwabana wafanyabiashara mkoani humo ni kuwaona wananchi wakisherehekea sikukuu hizo kwa kununua vyakula na vitu mbalimbali kulingana na bajeti waliyoitenga na si kuona wananchi wakiibiwa kwa kuuziwa vyakula kwa bei kubwa.
Hata hivyo Bi.Ishengoma amevipongeza vyombo vya habari mkoani iringa kutokana na mchango mkubwa wa kuleta maendeleo ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano katika katika kuwafichua wafanyabiashara wanaopandisha bei kiholela.
Mwisho..
Home »
» WANAOPANDISHA BEI ZA VYAKULA KIHOLELA KUKIONA CHA MOTO.
0 comments:
Post a Comment