TARIME.
MKUU wa Wilaya ya Tarime, Mkoa wa Mara, John Henjewele amesema kuwa
utoroshaji wa tumbaku kwenda nchi ya jirani ya Kenya ni hujuma kwa
uchumi wa nchi ambayo inazalishwa ndani ya nchi na kuuzwa na
kunufaisha nchi nyingine ama eneo lingine.
Kauli hiyo ilitolewa katika kijiji cha Nyabisaga kata ya Pemba
wilayani humo siku ya kufungua rasmi msimu wa ununuzi wa tumbaku
iliyofanyika wilayani Tarime na kusema kuwa kutoroshwa kwa zao hilo
kunasababisha nchi kukosa ushuru ambao unapaswa kulipwa eneo la
uzalishaji .
“Acheni mchezo wa kutorosha tumbaku nje ya nchi jengeni utamaduni wa
kuuzia mazao yenu ndani ya nchi kwa kitendo cha kutorosha huo ni
uhujumu wa uchumi wetu wa nchi kwani serikali inakosa mapato,”alisema
Henjewele.
Katika hatua nyingine wakulima wa tumbaku chini ya Katibu wao Rhobi
Kimayi wamesema kuwa hawataki kuuza tumbaku kwa dola kwa sababu
hawazijui na wanahisi wanaibiwa na Bodi ya Tumbaku Tanzania ( TTB)
Pia alisema kuwa kuna changamoto nyingi zinazowakabili wakulima hao ni
idadi ndogo ya wataalam wa tumbaku pia Licha ya kupata janga la mvua
za mawe bado mkulima analazimika kulipa deni lake la pembejeo
wanazokopeshwa na kampuni ya ununuzi ya Allince one Tanzania Tobacco
Company Limited (AOTTL).
Vile vile waliomba kuwa pindi tumbaku likiungua kampuni ione namna ya
kufuta au kupunguza mkopo sambamba na athari zinazowaathiri wakulima
kisaikolojia ama kuwakatisha tamaa kulima tumbaku.
Mwakilishi wa Bodi ya Tumbaku Stanley Mnozya iliahidi kufuatilia
suala hilo, kwa vile inaleta mchakanganyiko, iwaje pembejeo zikatwe
kwa badiliko la dola kubwa ili hali tumbaku iuzwe katika badiliko
dogo.
“Haifai kuuza kwa dola kwa vile wakulima wanauza katika exchange rate
tofauti, hiyo inawaonea baadhi ya wakulima na ni vema ikawa kwa kiasi
fulani kwa wakulima wote,”alisema Mnozya.
Pia aliwaasa wakulima kuwa matatizo ya dola yalikuwa na nia nzuri
lakini utekelezaji wake umekuwa na changamoto nyingi zinazotoa maana
halisi ya dola iliyokusudiwa.
Hata hivyo aliwaeleza wakulima kuwa tatizo hilo pia limejitokeza
kwa waziri wa kilimo alipokuwa ziarani tabora tarhe 14/11/2013 na
aliwaahidi wakulima kuwa suala hili la kuendelea kutumia ama kutotumia
dola litazingatiwa wakati wa upangaji wa bei mwakani.
MWISHO
Home »
» HENJEWELE ASEMA UTOROSHWAJI TUMBAKU NI HUJUMA
0 comments:
Post a Comment