Mez B
Mez B ni kati ya wasanii ambao walifanya kazi kwa
ukaribu sana na marehemu alberty
mangwea , (ngweah) na kufanikiwa
kutoa baadhi ya ngoma wakiwa pamoja
, amesema amejikuta akiuchukia sana muziki wa kitanzania baada ya ngwea kufariki tu , na hii ni badaa ya kuona kama amepoteza
kila kitu katika muziki kiasi cha wakati mwingine kujikuta na mfadhaiko (
stress) kila anapomkumbuka Ngweah.
Marehemu Albert Mangweah
Mez B
aliyasema hayo wakati akizungumza na blog
ya delduero .blogspot
.com kwa njia ya simu kuhusiana na mipango yake ya kimuziki na namna ambavyo amejipanga tena kwa mwaka huu baada ya mwaka jana kuachia ngoma iliyokwenda kwa jina la kidela .
“patty najua
unajua jinsi ambavyo mimi na marehemu cowboy
tulivokuwa , kwa hiyo kiukweli wakati mwingine nakuwa na stress sana
kila ninapomfikiria marehemu alberty mangwea , maana nahisi kifo chake kilinichanganya na
kunivuruga kimuziki kiasi cha mimi
kuona kama nimepoteza kila kitu
yaani katika hili
gemu.”alisema MEZ B
katika hilo
pia akiuzungumzia muziki wa Tanzania
kwa sasa na jinsi ulivyo , mez b
alisema muziki wa Tanzania kwa sasa ni
mzuri lakini haupo fair kabisa kiasi
cha kuendelea kuwaumiza wanaojua na kuwaacha katika mateso na hali ngumu ya kimaisha , kutokana uarasimu wa wachache wenye nguvu ya fedha
kuendelea kuhit hata kama ni
wabovu na wale wasio na fedha hata kama ni wazuri wakiachwa .
“Muziki hauko fair kabisa , ambao tunauwezo mkubwa
sana bado tunakuwa katika hali
ngumu ya kimaisha na hali ya umasikini
wa hali ya juu , lakini wale wasiokuwa na uwezo wa kufanya vizuri katika
gemu,lakini wana uwezo wa kifedha ndo hao wamekumbatia gemu na hakuna wachofanya zaidi ya kupewa
promo kiasi cha kuwaacha wasio na
uwezo wa kifedha kuzidi kuteseka au
kutokusikika , na patty nakwmabia kama hii hali itaendelea
inavyoendelea we jua tu muziki wetu kila siku tutakuwa tunayasikia yale
yale kutoka kwa wale wale”alisema Mez B
Marehemu Ngwea alifariki dunia may 28 2013 Johannesburg South
Afrika alikokuwa kwaajili ya kufanya show, ambapo kilikua ni kifo cha ghafla kwa sababu
usiku kabla ya kulala aliagana vizuri na Watanzania wenzake kijiweni tena
akaahidi kurudi Afrika Kusini baada ya kipindi cha Ramadhani.
Kabla ya kifo chake tayari Ngwea alitakiwa kurudi Tanzania lakini akaahirisha safari yake mara tatu mfululizo ili aendelee kuwepo Afrika Kusini ambako alimwambia Bushoke kwamba amepata mtu wa kumlipia ada hivyo angerudi Afrika Kusini hivi karibuni ili aanze masomo ya muziki.
0 comments:
Post a Comment