`

Home » » KITENGO CHA HABARI CHA UMOJA WA MATAIFA UNIC CHAENDELEA NA MASOMO YAKE KATIKA SHULE YA MSINGI DIAMOND YA JIJINI DAR.

KITENGO CHA HABARI CHA UMOJA WA MATAIFA UNIC CHAENDELEA NA MASOMO YAKE KATIKA SHULE YA MSINGI DIAMOND YA JIJINI DAR.


Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kimeendelea kutoa mafunzo na elimu juu ya umuhimu wa kukumbuka maadhimisho ya siku ya kumbukumbu ya ukombozi wa kambi za mateso ya Auschwitz kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi nchini.

Akizungumza na wanafunzi wa shule ya  msingi ya Diamond ya jijini Dar es Salaam leo asubuhi, Afisa habari wa kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama amesema kwamba ni muhimu kwa kizazi na kizazi kujifunza madhara ya mauaji na maangamizi ya moto dhidi ya wayahudi yaliofanywa na askari wa kinazi wa Ujerumani.

Alisisitiza kwamba mauaji na mateso ya Auschwitz yalipoteza mamilioni ya watu wasio na hatia na mafunzo haya yanaonyesha chuki na ubaguzi dhidi ya wayahudi na chuki za aina nyingine yoyote hazina nafasi katika ulimwengu wa leo.
Nkhoma amesema kwamba binadamu wote ni sawa na tofauti za kipato au dini au rangi haziwezi tena kujenga chuki dhidi ya binadamu wengine kwa sababu wote kama binadamu tuna haki sawa mbele za mungu.


Wakati huo huo, ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika siku ya kimataifa ya maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya maangamizi ya moto amesema aliona makambi ambako wayahudi, waroma, wasinti, mashoga, wafungwa wa kivita na watu wenye ulemavu walitumia siku za mwisho katika hali ya kinyama.
Afisa Habari wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond juu ya umuhimu wa kujifunza mauaji ya kimbari ya wayahudi ya mwaka 1933.
 Bi.Usia Nkhoma Ledama akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Diamond ya jijini Dar es salaam
Wanafunzi wa shule ya msingi ya Diamond wakimsikiliza bi. Usia Nkhome Ledama asubuhi ya leo.

                           
Baaadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Diamond wakisoma vijarida vilivyotolewa na na umoja wa mataifa. 

mwisho..............

CHANZO: MO BLOG.



0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK