`

Home » » THIAGO AFUNGA BONGE LA BAO BAYERN IKISHINDA 2-1 DHIDI YA STURTTGART

THIAGO AFUNGA BONGE LA BAO BAYERN IKISHINDA 2-1 DHIDI YA STURTTGART

BAO la tik tak la Thiago dakika za majeruhi limeipa Bayern Munich ushindi wa 2-1 dhidi ya Stuttgart na kuwawezesha The Bavarians kuendeleza wimbi la ushindi na kutulia kileleni mwa Bundesliga kwa pointi 13 zaidi.

Mspanyola huyo mwenye umri wa miaka 22 aliiwahi vizuri krosi ya Rafinha na kubinuka tik tak kuitumbukiza nyavuni dakika ya tatu ya muda wa nyongeza.

Mchezaji wa Bayern aliyetokea benchi, Claudio Pizarro alifunga kwa kichwa dakika ya 76 akimalizia mpira wa adhabu wa Thiago, hilo likiwa bao la kusawazisha baada ya Vedad Ibisevic kutangulia kuwafungia wapinzani wao dakika ya 29.

Bayern sasa imetimiza mechi 43 bila kufungwa Bundesliga ikiwa kileleni kwa pointi zake 50 baada ya kucheza mechi 18, mbele ya Bayer 04 Leverkusen yenye pointi 37 baada ya kucheza mechi 18 pia.

THIAGO AKIFUNGA BONGE LA BAO LA TIK TAK.

                                          THIAGO PICHANI AKISHANGILIA BAO LAKE

0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK