RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE AMEWASILI DAVOS, USWISI, JANA JIONI KWA AJILI
YA KUHUDHURIA MKUTANO WA MWAKA 2014 WA TAASISI YA UCHUMI DUNIANI YA WORLD ECONOMIC FORUM (WEF).
MKUTANO HUO WA SIKU NNE UMEANZA LEO HUKU
RAIS KIKWETE AKITARAJI KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA NIGERIA, BW. GOODLUCK
JONATHAN AMBAYE NCHI YAKE ITAANDAA MKUTANO WA WEF AFRIKA UTAKAOFANYIKA MEI
MWAKA HUU.
TANZANIA ILIKUWA NCHI YA KWANZA YA
AFRICA UKIACHA AFRIKA KUSINI KUANDAA WEF-AFRIKA ILIYOFANYIKA MNAMO MWAKA 2010.
AIDHA RAIS KIKWETE LEO ANATARAJI
KUHUDHURIA KIKAO MAALUM KUHUSU MAJI NA USALAMA WAKE DUNIANI KABLA YA KUKUTANA
NA NAIBU WAZIRI MKUU WA UINGEREZA MHE. NICK CLEGG HUKU AKITARAJI KUFANYA
MAZUNGUMZO NA MWENYEKITI NA MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA JETRO YA JAPAN, BW.
HIROYUKI ISHIGE.
MCHANA WA LEO, RAIS KIKWETE ALISHIRIKI
KATIKA KIKAO KILICHOKUWA NA MALENGO YA KUVUNJA VIKWAZO VYA MAENDELEO.
KATIKA ZIARA HIYO RAIS
KIKWETE AMEAMBATA NA MAWAZIRI WATATU AMBAO NI PROFESA JUMANNE MAGHEMBE AMBAYE
NI WAZIRI WA MAJI; WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA MHESHIMIWA CHRISTOPHER
CHIZA NA MHESHIMIWA HARRISON G. MWAKYEMBE, WAZIRI WA UCHUKUZI.
MWISHO.....
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DK KIKWETE JAKAYA
0 comments:
Post a Comment