`

Home » » ROSE NDAUKA APATA MTOTO WA KIKE

ROSE NDAUKA APATA MTOTO WA KIKE


Msanii wa filamu, rose ndauka amejifungua mtoto wa kike jumapili iliyopita katika hospitali ya taifa ya muhimbili, dar es salaam na kusisitiza, amefanana na baba yake.

Ndauka ambaye miezi michache iliyopita, alitangaza kusimama kuigiza kwa muda wa mwaka mmoja ili ajitathmini alijifungua mtoto huyo kwa operesheni.

Katika mazungumzo na mwanaspoti, ndauka alisema: “namshukuru mungu, nimefanikiwa kujifungua salama, mtoto mwanamke.”

“ni faraja kwangu kwa sababu nimepata mwenzangu na amefanana na baba yake mzazi ambaye anaonekana akiwa naye katika (picha,” alisema ndauka bila kutaja jina la baba wa mtoto huyo.

Ndauka ni mwigizaji maarufu wa filamu anayekubalika katika tasnia hiyo huku akitamba na kazi zake mbalimbali zikiwamo, bad girl, fall in love na nyinginezo.

CHANZO: MWANASPORT.

                          NDAUKA NA BABA WA MZAZI MWENZAKE. 





0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK