`

Home » » WANANCHI KALENGA WAMLILIA MGIMWA.

WANANCHI KALENGA WAMLILIA MGIMWA.

Na Brdina Majinge

Iringa.

WAKAZI wa jimbo la Kalenga lililopo wilaya ya iringa vijijini mkoani iringa wamepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa waziri wafedha nchini na mbunge wa jimbo hilo william mgimwa aliyefariki dunia jana akiwa katika matibabu nchini afrika kusini.
          
Akizungumzia namna alivyoguswa na msiba huo mwenyekiti wa halmashauri ya iringa Bw. Steven Mhapa alisema kuwa halmashauri imepata pigo kumbwa kutokana na mchango wake katika kuisaidia jamii nakusema kuwa wamempoteza mtu mwenye busara na mchapa kazi kutokana na ushirikiano alikuwa akitoa kwa halmashauri hiyo katika kuwatafutia wafadhili kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Naye Bw. Raphael Lengesia mmoja wa wakazi wa jimbo lililokuwa likiongozwa na marehemu mgimwa alisema baada ya kusikia taarifa za kifo cha mbunge huyo waligubikwa na mshtuko mkubwa na kusema kifo hicho kimeacha pengo kubwa kwa wakazi hao.

Lengesia aliongeza kuwa marehemu alikuwa mtetezi katika masuala mbalimbali likiwemo ufunguzi wa barabara, shule, zahanati na hasa katika suala la maji alikuwa akilipigia kelele na tumepata maji katika kijiji hicho, pia wananchi wataendelea kumkumbuka kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya kwa kuwa alikuwaakiwathamini sana wananchi wake.

Mwisho…

MGIMWA WAKATI WA UHAI WAKE
.




0 comments:

Post a Comment

 
Designed By | Wishes co |
Copyright © 2014. Jicho La Mdadisi - All Rights Reserved
Template Modify by
Proudly powered by Wishes INK