Rais wa jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete,ameuzindua mkoa rasmi wa Simiyu na kuwapongeza wananchi wa mkoa huo kwa uamuzi wao wa kujenga Benki ya wananchi wa mkoa Simiyu.
Amesema hatua hiyo itachochea fursa ya upatikanaji wa mitaji ili kukuza wa uchumi na kupunguza umasikini unawakabili miongoni mwa wananchi wa mkoa huo.
Rais Kikwete amepongeza hatua ya wananchi kuchangishana fedha na kuwekeza katika huduma ya fedha kwa kuanzisha Benki hiyo ikiwa ni miongoni mwa benki za 40 zilizopo nchini huku akisema amejisikia faraja kweli kwa hatua hiyo.
Katika uzindizi huo rasmi wa mkoa mpya wa Simiyu mjini Bariadi,umefanyika sanjari na uwekeji wa jiwe la msingi kwa benki ya wananchi wa mkoa huo,huku Rais Mh Dk Jakaya Mrisho Kikwete,akitumia nafasi hiyo kuwapongeza wananchi hao kwa kujiunga pamoja na kuanza mchakato wa kufungua benki yao ambayo amesema itasadia kuharakisha maendeleo ya mkoa huo mpya.
Akisoma taarifa kwa Rais Jakaya Kikwete ya kuanzishwa kwa benki ya wananchi wa mkoa simiyu,mwenyekiti wa bodi wa benki hiyo Eng Christopher Sayi,amesema baadhi ya wananchi wa mkoa huo,walianza mchakato wa kuanzishwa kwa benki ili kusogeza huduma nzuri za kibenki kwa wananchi pia itumike kuchochea uchumi wa wananchi wa mkoa huo mpya, ambao wengi wanajishughulisha na shughuli za kilimo, ufugaji, uchimbaji wa madini uvuvi na biashara za viwanda.
Kwa mujibu wa kamati ya uanzishwaji wa benki hiyo,tayari kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 1.8 kimepatikana huku kamati hiyo ikitekeleza ushauri wa rais kikwete wa kuhamasisha wananchi wengi zaidi kununua hisa na hivyo kupanua wigo mpana wa wananchi kumilikiwa benki hiyo, badala ya watu wachache,wakati mikakati ni kufungua matawi zaidi katika wilaya zote za mkoa wa Simiyu na mikoa jirani.
mwisho..............
0 comments:
Post a Comment